12 August 2014

MAJAMBAZI YAUA MKE NA MUME,


Watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamiana kuwaua mume na mke na kumjeruhi mtoto mchanga mwenye umri wa miezi 4 aliyeachwa na mama yake aliyeuliwa katika tukio lililotokea kijiji cha Murvyagira wilayani Ngara mkoani Kagera Ijumaa ya Agost 08,2014.

Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu amesema majambazi hao walivamia nyumbani kwao majira ya saa 3 usiku ambapo walitumia panga na jembe kuwaua baba na mama yake na kisha kuwapora Maharage gunia moja, Radio, Gunia la Karanga, Mabati na Fedha vitu ambavyo hadi sasa thamani yake haijajulikana, huku wahalifu hao wakitokomea kusikojulikana.

Aidha baadhi ya wananchi walioongea na Blog hii, wameomba juhudi ya kuimarishwa hali ya usalama na ulinzi wilayani Ngara izidishwe hasa wakati huu ambako matukio ya mauaji yamezidi kujitokeza. PICHA ZAIDI>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname