Akiongea na tovuti ya Times Fm kupitia simu ya Afande Sele, msimamizi wa kazi za Afande Sele aliyejitambulisha kwa jina la Jackson Busanda amesema kuwa mama Tunda alifariki kutokana na ugonjwa wa malaria uliomsumbua kwa muda wa siku tatu.
“Alilazwa katika hospitali ya St. Mary Morogoro akatolewa jana lakini usiku hali yake kidogo ilizidiwa akapelekwa hospitali kubwa ya Morogoro na umauti ukamkuta hapo. Aliugukua kwa muda wa kama siku tatu.” Jackson Busanda ameiambia tovuti ya Times Fm.
Akizungumzia hali ya Afande Sele kwa sasa, amesema kuwa Afande Sele alizimia baada alipokuwa anaenda kuuona mwili wa marehemu.
Kuhusu utaratibu wa mazishi, amesema kuwa familia imepanga kufanya mazishi leo majira ya saa tisa mchana katika makabuli ya Kola, mjini Morogoro.
Marehemu ameacha watoto wawili ambao ni Tunda na Sanaa.
Tunampa pole Afande Sele, tunamuombea apate nguvu ya kuvuka kipindi hiki kigumu.
Mama Tunda apumzike kwa amani. Amina.
Afande aliandika ujumbe kwenye Facebook na Instagram kutoa taarifa ya msiba huo.
No comments:
Post a Comment