19 July 2014

YATAKA MOYO...MAUZAUZA KABURI LA RECHO WA BONGO MOVIE...CHEKI HIRIZI NA NAZI ZIKIWA KABURINI

AMA kweli duniani imani  imekwisha! Ikiwa inakaribia miezi miwili tangu kifo cha msanii wa filamu Bongo, Rachel Leo Haule, vitu vya kutisha vinavyoashiria mambo ya uchawi vimekutwa juu ya kaburi lake, Kinondoni jijini Dar.
Tunguli za kichawi zikiwa juu ya kaburi la Marehemu Recho Haule.
Tukio hilo la kustaajabisha, lilidaiwa kutokea Alhamisi iliyopita katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Kwa mujibu wa chanzo chetu, ndugu wa marehemu mmoja ambaye hakujulikana jina walikuwa kwenye makaburi hayo wakifanya kumbukumbu mbalimbali ndipo walipokuta ‘madongoloji’ hayo juu ya kaburi la Recho.
Muonekano wa tunguli hizo kwa karibu zaidi.
SIMU YAPIGWA GLOBAL
Baada ya mpashaji huyo naye kushuhudia mauzauza hayo alipiga simu kwenye Ofisi za Global Publishers inayochapisha magazeti pendwa ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani na Ijumaa na kupokelewa na  kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ambapo alimweleza mkuu wa zamu hali ilivyo juu ya kaburi hilo.
toa habari: “Jamani hapo ni Global?” 
OFM: “Ndiyo. Tukusaidie?”
Mtoa habari: “Kama mnaweza, njooni kwenye Makaburi ya Kinondoni haraka sana. Juu ya kaburi la Recho kumewekwa vitu kama vya ushirikina.”
OFM: “Tupe dakika sifuri tu.”
Mama aliyefika kaburini hapo akishudia tunguli hizo.
OFM WATINGA NA PIKIPIKI
Kama kawaida mkuu wa zamu aliwatuma mapaparazi wake wanaotumia pikipiki ziendazo kasi ambao walikwenda mpaka eneo la tukio na kukuta vitu hivyo ambavyo ni tunguri moja iliyoviringishwa shanga, kitambaa cha kanga chakavu, manyoya ya kuku, yai moja (huenda likawa viza) na vitu vingine ambavyo havikujulikana ni nini. 

WALINZI WATAFUTWA Baada ya kujionea vitu hivyo, mapaparazi wetu walikwenda kuwauliza walinzi wa makaburi hayo kama walikuwa na taarifa hizo.Mlinzi mmoja aliyeonekana kuwa ni fundi wa kuzungumza lakini bingwa wa uoga, hasa kwa kuona mauzauza ya kutisha kama hayo ndiye aliyepatikana. Akasema:
Mmoja wa vijana waliofika kaburini hapo na kushuhudia tukio hilo.
“Ah! Hivyo vitu vimetupwa na nani? Kuna watu walikuwa wakitembelea makaburi ya ndugu zao ina maana hawakuviona hivyo vitu?
“Lakini huyo mtu aliyewapigia simu mngemuuliza yeye, anaweza kuwa aliwaona walioviweka.  Mimi siwezi kwenda sasa hivi kwenye hilo kaburi.” 

NDUGU WA MAREHEMU WENGINE Ingawa mlinzi huyo alishindwa kwenda kushuhudia tukio hilo, lakini watu  waliokuwa wakisafisha makaburi ya ndugu zao walifika kwenye kaburi hilo kujionea madongoloji hayo.
Miongoni mwa waliofika na kuwa mashuhuda ni mama mmoja aliyedai ni  mlokole wa Kanisa la KKKT Usharika wa Kimara- Temboni jijini Dar ambaye alikataa kutaja jina lake.

Mlokole huyo alivikemea vitu hivyo kwa Jina la Yesu kisha akasema havina tena mamlaka  ya kishetani kwa wakati huo na vimebaki kuwa takataka baada ya kuvipiga Neno la Mungu.
Mtu aliyekuwa akifanya usafi kwenye makaburi hayo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
BABU ASEMA NI NDUMBA
Shuhuda mwingine alikuwa ni kijana mmoja aliyekwenda kujengea kaburi la mteja wake ambaye alishtushwa na mauzauza hayo na kusema hali inatisha! Baada ya kijana huyo, babu mmoja aliyekutwa eneo hilo alisema vitu hivyo ni ndumba maarufu sana mkoani Tanga ambapo alisema anaifahamu ndumba hiyo ambapo wachawi walikwenda kuwangia kaburi hilo na kujaribu kuivuta nyota ya marehemu. 

Babu huyo aliongeza kuwa, wachawi hao walichelewa kwani kwa kawaida kafara kama hiyo hufanywa siku saba baada ya mwili wa marehemu kuzikwa. “Mara nyingi nyota za wafu huweza kutumiwa na watu walioko duniani ingawa wakati mwingine mtumiaji wa nyota hiyo anaweza kupatwa na madhara makubwa ikiwemo kifo cha ghafla.
“Hawa ni cha mtoto tu, walikuja kulichezea hili kaburi lakini wamechemsha,” alisema mzee huyo.
Marehemu Recho Haule akiwa na Mpenzi wake, Saguda enzi za uhai wake.
SAGUDA WA RECHO SASA
Baada ya hapo, mapaparazi wetu walimsaka aliyekuwa mchumba wa marehemu Recho, George Saguda ambaye alisema wao kama familia hawahusiki na tukio hilo na kudai hiyo itakuwa ni mipango ya washirikina.
Saguda akaenda mbele zaidi kwa kusema: ”Nitakwenda kukutana na walinzi wa makaburi wanieleze kinagaubaga kulikoni kaburi la mchumba angu kuchezewa hivyo.”

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname