Diamond akihojiwa muda mfupi baada ya kushinda tuzo AFRIMMA
Zinaitwa African Muzik Magazine Awards ambapo za mwaka huu 2014
zimetolewa huko Eisemann center Texas Marekani na kuhudhuriwa na mastaa
mbalimbali akiwemo Diamond wa Tanzania ambae pia alikua mmoja wa
wanaowania tuzo.Good news za ushindi wote huu ni kwa mujibu wa meneja Babu Tale ambae nae kahudhuria tuzo hizi Marekani alienitumia msg kwa kusema Diamond ameshinda tuzo mbili moja ya Msanii bora wa Afrika Mashariki na nyingine ni wimbo bora wa kushirikiana ambao ni ‘number one rmx’ alioufanya na Davido wa Nigeria.
Babu Tale ameendelea kusema japo kwenye tovuti ya AFRIMMA Diamond katangazwa mshindi wa tuzo moja, ukumbini walipohudhuria Diamond katangazwa mshindi wa tuzo mbili.
Kolabo bora ni tuzo iliyokua inawaniwa na single ya T Pain na 2 Face – rainbow, Khona ya Uhuru na Mafikizolo wa South Africa, Surulere remix ya Dr Sid wa Nigeria, Mkenya Amani ft. Waganda Radio na Weasel ‘kiboko changu’ J Martins ft. Dj Arafat ‘touching body’ na Rebees na Wizkid ‘slow down’
Tuzo ya msanii bora wa kiume Afrika Mashariki aliyoishinda Diamond ilikua inawaniwa pia na Ben Pol kutoka Tanzania, Bebe Cool wa Uganda, Wyre wa Kenya, Navio wa Uganda na Jackie Gosee wa Ethiopia.
Lady Jaydee ameshinda tuzo ya Msanii bora wa kike Afrika Mashariki aliyokua anashindania na Rema wa Uganda, Aster Aweke wa Ethiopia, Avril wa Kenya, Victoria Kimani wa Kenya na Irene Ntale wa Uganda.
Producer bora wa mwaka tuzo yake imechukuliwa na Mtanzania Sheddy Clever aliekua anashindana na Don Jazzy wa Nigeria, Shizz wa Nigeria, Killbeatz wa Ghana, Oskido wa South Africa, Nash Wonder wa Uganda na Ogopa wa Kenya.
Tuzo yaMtayarishaji bora wa video imekwenda kwa Ogopa Dj’s ambao ndio waliifanya ile video ya kwanza ya ‘My number 1′ ya Diamond Platnumz.
Stori zaidi na pichaz vitafata baadae hivyo endelea kukaa karibu na Kandili Yetu Blog mdau ili ujue kilichotokea kwenye tukio hili ambalo limewahusisha wakali wengine kama Davido, 2Face, Fally Ipupa, Iyanya, Flavour, Wyre, Miriam Chemmoss na wengine ambao ni sehemu ya watu kutoka nchi 17 za Afrika.
No comments:
Post a Comment