10 July 2014

UNAWAJUWA FREEMASON NA SIGN ZAO PAMOJA NA HARAKATI ZA KIDINI DUNIANI .....INGIA HAPA KUJUA

Hatimaye mbegu ya ‘tamaa’ iliyopandwa na rais Nimrodi wa serikali ya awamu ya kwanza ilipotengeneza‘mimba’ na kuzaa mtoto ‘dhambi’, mtoto huyo alikomaa baada ya kufikisha umri wa utu uzima. Sasa hakuitwa ‘mtoto’ tena bali jina lake lilibadilika na kuitwa‘mauti’. Kumbuka kwamba kuna hatua nne za kukua na kukomaa kwa mbegu hadi wakati wa kuvunwa. Hivyo ndivyo ilivyokuwa wakati dunia yetu iliposhuhudia awamu nne za serikali moja ya dunia ambapo katika awamu ya nne palitokea mavuno yaliyoleta mazao ya muungano wa serikali na dini.


Ulikuwa ni utawala wa serikali ya awamu ya nne (Roman empire) chini ya rais Constantine aliyeweka ikulu yake huko Roma ndipo imani ya kweli ilipokufa baada ya rais huyo kuanzisha dini iliyochanganya ukweli na uongo kwa kutumia kanuni ya‘Thesis x Antithesis = Synthesis. Imani ya kweli ilikuwa ni ‘Thesis’ wakati imani ya kipagani iliyoanzishwa na Nimrodi ilikuwa ni ‘Antithesis’. Imani hizi mbili zilichanganywa na rais Constantine na kuzaa kitu kinachoitwa ‘Synthesis’ yaani mchanganyiko wa ukweli na uongo. Hiyo ilikuwa ni baada ya miaka mingi kupita tangu rais Nimrodi alipotamani kuanzisha mfumo wa utawala uliunganisha serikali na dini na kuwa kitu kimoja. Hiyo ilikuwa ni awamu ya nne ya utawala wa serikali moja ya dunia. Naam! Dini iliyoanzishwa huko Roma wakati wa awamu ya nne ya utawala wa serikali moja ya dunia chini ya rais Constantine ilikuwa ni matokeo ya mbegu ya ‘tamaa’ ya rais Nimrodi ya kuanzisha mfumo wa serikali iliyoungana na dini katika utawala wa dunia nzima.


Jambo hilo la kuunganisha serikali na dini pamoja na kuchanganya ukweli na uongo lilipigwa vita vikali na ‘waprotestant’ ambao hawakuwa tayari kuona ukweli wa neno la Mungu ukichanganywa na uongo. Hata hivyo ‘waprotestant’ hao hawakufanikiwa kutenganisha serikali na dini na ndipo wakamua kujitenga na dini iliyokuwa imeungana na serikali ili wapate kumuabudu Mungu katika roho na kweli.


Ilipofika mwaka 1798 kulitokea badiliko katika serikali iliyoungana na dini baada ya rais na kiongozi wa dini kukamatwa na kuuawa huko ufaransa. Baada ya kifo cha rais na kiongozi wa dini wa serikali moja ya dunia, ilionekana kana kwamba ndio mwisho wa mfumo wa utawala uliounganisha serikali na dini. Lakini haukuwa mwisho kwa sababu liliundwa taifa moja katika mji wa Roma likiwa linaendeleza mfumo wa kuunganisha serikali na dini. Taifa hilo likapewa jina la Vatican. Ndioo! Vatican ni nchi inayotawalaiwa na Papa akiwa ndiye rais na kiongozi wa dini pia. Sasa jina la serikali hiyo likaitwa ‘Roman Catholic’ yaani ‘ulimwengu wa Kirumi’. Maana ya neno ‘catholic’ ni ‘universal’ au iliyoenea dunia nzima. Serikali hii imeenea dunia nzima kutokana na uwepo wa wawakilishi (mabalozi) wa taifa hilo duniani kote. Ukilinganisha na mataifa mengine katika eneo la mraba, inawezekana taifa hili ndilo dogo kuliko mataifa mengine duniani kote lakini ni taifa lenye nguvu kubwa kuliko mataifa yote – usishangae!


Zimekuwepo juhudi za kuhakikisha kwamba dunia nzima inarudi kwenye mfumo wa utawala wa serikali na dini. Freemasons wamekuwa kwenye mipango ya muda mrefu latika kuhakikisha kwamba serikali moja ya dunia itakayounganisha dini na uchumi kwa pamoja inaundwa haraka iwezekanavyo. Serikali hiyo itakuwa imejengwa kwenye msingi uliowekwa na rais wa kwanza katika awamu ya kwanza ya utawala wa serikali moja ya dunia. Itakumbukwa kwamba rais Nimrodi alianzisha dini iliyoabudu miungu (sayari) 36 ambapo jumla ya miungu hao ilileta namba 666.
..... Safari ijayo tutaitazama namba 666 na uhusiano wake na Freemasons

Sasa msikilize muumini wa freemason na mfanyabiashara za kibenki bwana Paul Warburg akisema kwamba "We will have a world government whether you like it or not. The only question is whether that government will be achieved by conquest or consent." (maneno hayo aliyasema siku ya February 17, 1950, alipokuwa akilihutubia baraza la Seneti nchini Marekani).Warburg alimaanisha kwamba serikali ya dunia lazima ianzishwe, utake au usitake. Swali ni kama serikali hiyo itaanzishwa kwa makubaliano au kwa vita.


Mwaka 1992, Dr. John Coleman aliandika kitabu kinachoitwa ‘Conspirators Hierarchy: The Story of the Committee of 300’. Katika kitabu hicho Dr. Coleman anaainisha watu wanaohusika na mchakato mzima wa kuundwa kwa serikali moja ya dunia au New World Order. Katika ukurasa wa 161 Dr. Coleman anaelezea malengo ya kamati ya watu 300 (mwenyekiti wake akiwa ni mkuu wa kanisa duniani) na kusema:"A One World Government and one-unit monetary system, under permanent non-elected hereditary oligarchists who self-select from among their numbers in the form of a feudal system as it was in the Middle Ages. In this One World entity, population will be limited by restrictions on the number of children per family, diseases, wars, famines, until 1 billion people who are useful to the ruling class, in areas which will be strictly and clearly defined, remain as the total world population.


There will be no middle class, only rulers and the servants. All laws will be uniform under a legal system of world courts practicing the same unified code of laws, backed up by a One World Government police force and a One World unified military to enforce laws in all former countries where no national boundaries shall exist. The system will be on the basis of a welfare state; those who are obedient and subservient to the One World Government will be rewarded with the means to live; those who are rebellious will simply be starved to death or be declared outlaws, thus a target for anyone who wishes to kill them. Privately owned firearms or weapons of any kind will be prohibited."


Kwa ufupi maneno hayo yanamaanisha kwamba kutakuwepo na serikali moja na mfumo mmoja wa kifedha ambapo kiongozi wa serikali hiyo atachaguliwa na watu 300 wanaounda kamati kuu ya serikali hiyo. Idadi ya watu duniani itapunguzwa kwa kuanzishwa sharia za kuwa na idadi maalumu ya watoto katika familia ambapo mbinu itakayotumika kutekeleza lengo hilo ni kusababisha magonjwa, vita, njaa hadi idadi ya watu ifikie bilioni moja duniani kote. Kutaanzishwa mfumo mmoja wa kijeshi utakaosimamia sharia katika nchi zote ambapo mipaka yote ya nchi zote itaondolewa. Wale watakaokuwa watiifu katika serikali hiyo watawezeshwa kuishi; wale watakaokuwa wapinzani na waasi wataanchwa wafe kwa njaa au kuhumiwa kama wavunja sharia. Haki ya kumiliki silaha za aina yoyote itaondolewa’. Itakumbukwa kwamba hivi karibuni watoto 20 na waalimu wao 6 waliuawa kwa kupigwa risasi katika shule moja huko Marekani. Baada ya tukio hilo serikali ya Marekani imeanza kupitia upya sheria za umiliki wa silaha kwa watu binafsi.


Rais Barack Obama aliyeshinda uchaguzi ulioshirikisha vyama 6 nchini Marekani amekwisha saini mabadiliko kadhaa ya sheria. Rais Obama amesaini sheria inayoitwa TARP (Troubled Asset Relief Program) ambapo chini ya sheria hiyo mabenki yote (Wall street) pamoja na mabenki ya kigeni yanakuwa katika dhamana kwa serikali. Sheria nyingine ni H.R 347 (House Resolution) au “Federal Restricted Buildings and Grounds Improvement Act of 2011,”. Sheria hii inazuia maandamano ya kwenda kwenye majengo ya serikali ikiwa ni pamoja na zuio la kuendeleza majengo na ardhi. Wanaharakati wa haki za binadamu nchini Marekani (American Civil Liberties Union –ACLU)) wanaipinga vikali sheria hiyo kwamba inawagandamiza wanyonge. Sheria nyingine ni‘National Defense Authorization Act’ – NDAA. Sheria hii inampa nguvu na mamlaka rais wa Marekani kuamuru kukamatwa na kufungwa gerezani kwa mtu yeyote bila hata ya kufikishwa mahakamani na kufunguliwa mashitaka. Kama ulikuwa unafikiri kwamba rais Morsi Mohamed wa Muslim Brotherhood Misri amejipatia madaraka makubwa kupita kiasi, basi yupo pia rais wa Marekani chini ya NDAA!


Najua wengi watanishangaa ninaposema kwamba uchaguzi wa rais Marekani ulishirikisha vyama 6 na sio viwili. Ili usiniulize maswali juu ya hilo, vyama hivyo ni: 1)Democratic –Baraka Obama; 2)Republican – Miti Romney; 3)Libertarian Party - Gary Johnson; 4) Green Party- Jill Stein; 5) Constitution Party - Virgil Goode; na 6) Justice Party - Rocky Anderson.Kwa nini vyama 6 – ni namba ya utawala wa freemason.Kwa nini vyama vingine havikusikika? Ni kwa sababu Illuminati ndio walioshikilia ‘media’ na wao ndio waamuzi wa nani atangazwe na nani hapana.


Nini maana ya wito wa kuundwa kwa ‘world community’ pamoja na ‘Central World Bank’ kutoka kwa Papa Benedict xvi? Ni kutimizwa kwa unabii wa Ufunuo 13:17. Haitawezekana kuzuiwa kuuza na kununua kama hakuna chombo kinachosimamia uchumi na fedha. Chombo hicho ni ‘Central World Bank’ (CWB). Lakini pia CWB haitakuwa na nguvu za kusimamia shughuli za kifedha kama hakuna serikali nyuma yake. Serikali hiyo ni ‘World Community Authority’ au ‘World Government’ yaani serikali ya dunia.


Wakati Papa Benedict xvi akitoa wito wa kuleta ‘haki na amani’ duniani, chuo kikuu cha Kiislamu (Sunn Al - Azhar University) kimetoa shukrani kwa Vatican kutokana na juhudi za kanisa Katoliki kwa kukemea vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani duniani, kutetea imani za watu wote pamoja na kuziwezesha dini zote kutumia alama na nembo kama utambulisho wa dini husika.


Akihojiwa na waandishi wa habari, Mahmoud Azab ambaye ni mshauri wa Sheikh anayesimamia kitengo cha mahusiano ya kidini (interfaith Dialogue) katika chuo kikuu cha Al-Azhar, aliwashukuru wote wanaotetea ukweli na heshima ya dini. Mahmoud Azab alikuwa akijibu hotuba iliyotolewa hapo kabla na msemaji wa Vatican Fr. Federico Lombardi. Kwa nini Mahmoud atoe shukrani kwa Papa kutokana na matumizi ya alama/nembo katika dini? Unaweza kuchunguza alama/nembo kwenye jengo la chuo kikuu cha Al-Azhar na jengo alipokaa Papa Benedict xvi akihutubia baraza la haki na amani Vatican. Unazikumbuka kanuni 3 wanazotumia freemasons kufanya kazi zao? Tafakari!


Itakumbukwa kwamba baada ya kushambuliwa kwa ubalozi wa Marekani mjini Benghazi na kuuawa kwa aliyekuwa balozi wa Marekani nchini Libya kutokana na hasira za waumini wa kiislamu zilizotokana na kutolewa kwa sinema inayomkashifu SAW Mohammad (Innocence of Muslims), Fr. Federico Lombardialitoa matamko na kusema kwamba: “profound respect for the beliefs, texts, outstanding figures and symbols of the various religions is an essential precondition for the peaceful coexistence of peoples”akiwa anamaanisha kwamba ili pawepo na amani kwa watu, kunatakiwa pawepo na kuheshimu imani, maandiko pamoja na alama/nembo mbalimbali zinazotumiwa na dini kama utambulisho wao.


Akielezea kwa nini pamekuwepo na mjadala kati ya Al-Azhar University na Vatican, Abdel Muti al-Bayoumi, mjumbe wa ‘Islamic Research Academy’ katika chuo kikuu cha Al-Azhar alisema kwamba mjadala huo hauhusiani na kauli ya Papa Benedict xvi aliyoitoa kwa kuwatetea Wakristo wa dhehebu la Christian Copts wa Misri ambao wamekuwa katika wakati mgumu kutokana na kushambuliwa kwa sababu ya imani yao. Alipoulizwa kutoa kauli juu ya mjadala kati ya pande hizo mbili, Mahamoud Azab alisema, ““I have nothing to say on the subject at this present time” akimaanisha kwamba hawezi kusema juu ya mjadala huo kwa wakati huu. Hata hivyo Azab alikemea vikali vitendo vinavyofanywa na baadhi ya waumini kwa kuchoma Biblia wakati wa maandamano yaliyofanyika kupinga sinema ya ‘Innocence of Muslims’.Aliwataka waislamu wote kuheshimu Torah, Injili na maandiko Matakatifu kwa sababu ndivyo alivyofanya mtume Mohammad SAW.
Kwa nini pawepo na mfululizo wa mijadala kati ya Al-Azhar University na Vatican; serikali ya Iran na Vatican na hata serikali ya Saud Arabia na Vatican?


Awamu ya pili ya serikali ya dunia iliitwa Mede/Uajemi ambapo mmoja wa marais wa serikali hii aliitwa Dario.Eneo la sasa yalipokuwa makao makuu ya serikali hii ni Iran ya leo. Awamu ya tatu ya serikali ya dunia iliitwa serikali ya Uyunani au Greece government. Mmoja wa marais mashuhuri katika serikali hii alikuwa ni Alexander mkuu (Alexander the Great). Awamu ya nne ya serikali ya dunia iliitwa‘Roman Empire’ au himaya ya Roma. Mmoja wa marais wa serikali hii alikuwa ni Constantine. Serikali hii ndiyo iliyotawala kwa muda mrefu kuliko serikali zote zilizoitangulia.

Wakati serikali hizo zinatawala dunia, dini ya kweli ilikuwa haijatikiswa hadi serikali ya Roma ilipoanza kutawala. Je, dini ya freemasons ilianza lini? Ukiondoa dini aliyoianzisha Mungu katika bustani ya Edeni, dini ya freemasons ndiyo dini iliyoanza siku nyingi kuliko dini nyingine.Dini hii ilianzishwa pia kwenye bustani ya Eden mwanzilishi wake akiwa ni Shetani. Alimtumia Kaini anayejulikana kwa freemasons wa leo kama ‘first freemason’ yaani mjenzi huru wa kwanza.

Hatimaye rais Constantine kwa nusu aliamua kuachana na ibada za kipagani na kujiunga na Ukristo. Hii ilikuwa ni kutimizwa kwa andiko la 2 Wathesalonike 2:3,4 maana ulikuwa ni ukengeufu wa kanisa la mitume sehemu ya kwanza uliopelekea kuanzishwa kwa dini iliyochanganya ukweli na uongo. Kwa nini dini hii ilisubiri hadi awamu ya nne ya serikali ya dunia? Pengine nizungumzie kidogo maana ya namba nne kama inavyotumiwa na Mungu. Namba nne sio namba maalumu kwa freemasons lakini ni muhimu sana kwa Mungu. Namba nne inamaanisha kukomaa kwa mavuno na kuvunwa. Tazama hapa: “Akawaambia ufalme wa Mungu, mfano wake ni kama mtu aliyemwaga mbegu juu ya nchi…..Maana nchi huzaa yenyewe, kwanza jani, tena(pili)suke, kisha(tatu),ngano pevu katika suke. Hata (nne)matunda yakiiva mara aupeleka mundu, kwa kuwa mavuno yamefika” Marko 4:26 –kwenye mabano ni ufafanuzi wa mwandishi. Hizo ni hatua nne kufika kuvunwa kwa mbegu njema. Vipi habari ya mbegu mbaya? “Lakini kila mmoja hujaribiwa(kwanza)kwatamaa yake mwenyewe. Halafuile tamaa ikisha kuchukuamimba(pili), huzaa dhambi (tatu),na ile dhambi ikiisha kukomaa, huzaa mauti(nne)”Yakobo 1:14,15. Unaweza pia kujua ni kwa nini waisraeli walitumia miaka 40 (4x10) kutoka Misri hadi Kanaani; kwa nini Yesu, Musa walifunga kwa siku 40 (4x10). Kumbuka kwamba namba 10 kwa Mungu inawakilisha ‘ukamilifu wa Mungu’ na namba 7 inawakilisha ‘utimilifu wa Mungu’.Kuna tofauti kati ya ‘ukamilifu’ – ‘perfection’ na ‘utimilifu’ – ‘fulness’.Kitu kinaweza kuwa ‘timilifu’ lakini kisiwe ‘kamilifu’ lakini kitu hakiwezi kuwa ‘kamilifu’ bila ya kuwa ‘timilifu’. Kwa mfano mapigo 7 ni utimilifu wa ghabu ya Mungu lakini ukamilifu wa hukumu yake utafikiwa wakati Shetani, dhambi na wadhambi watakapoangamizwa motoni. Mungu alitoa amri 10 kwa wanadamu ikimaanisha kwamba amri hizo zinawakilisha tabia ya Mungu ambayo ni ‘kamilifu’. Lakini pia tunasoma “….Wewe wakitia muhuri kipimo, umejaa hekima na‘ukamilifu’ wa uzuri” kisha anaanza kutaja ni kwa namna gani alikuwa ‘mkamilifu’ wa uzuri akisema “1)Akiki, 2)Yakuti manjano, 3)Almasi, 4)zabarajadi, 5)shohamu, 6)Yaspi, 7)yakuti samawi, 8)zumaridi, 9)baharamani na 10)dhahabu. Lusifa alikuwa‘mkamilifu wa uzuri’ kutokana na kuvikwa aina 10 za madini ya thamani kubwa. Mungu ni‘mkamilifu’ kutokana na kuwa na tabia inayoelezewa kwenye amri 10katika Kutoka 20:4-17. Je wewe ni mkamilifu wa tabia kama ya Mungu kwa kuzitunza amri 10? Tafakari!

FREEMASONS NA FAMILIA 13 ZA ILUMINATI

 ceremonies. Lutherand his followers did not invent the reformed religion. They simply accepted it as presented by Christ and the apostles." E.G. White, Review and Herald, vol. 2, 48, col. 2.Hapo anamaanisha kwamba ‘Kristo (Yesu) alikuwa ni Mprotestant….wanamatengenezo waliiga kutoka kwa Kristo na mitume. Walijitenga na dini ya desturi na sherehe. Luther na wafuasi wake hawakuanzisha dini ya matengenezo. Waliikubali kama ilivyoonyeshwa na Kristo na mitume’ [rejea: R&H, Vol. 2, 48, col.2].

Ni kwa namna gani Kristo alijitenga? E. White anaendelea kusema: “Pharisees and Sadducees were alike silenced. Jesus summoned His disciples, and prepared to leave the temple, not as one defeated and forced from the presence of his adversaries, but as one whose work was accomplished. He retired a victor from the contest”. {DA 620.2}

‘Mafarisayo na masadukayo walinyamazishwa. Yesu aliwakusanya wanafunzi wake, na akawaandaa kuliacha hekalu, sio kama aliyeshindwa na kulazimishwa kuondoka kwa maadui zake, bali kama ambaye kazi yake ilikuwa imekamilika. Alikuwa ni mshindi katika mashindano”. {DA 620.2}

Biblia inasema kwamba Yesu alijitahidi kupingana na mafarisayo na masadukayo akiwa ndani ya mfumo wa dini ya kiyahudi na sasa alikuwa amefikia mwisho wa upinzani wake na akaamua kujitenga moja kwa moja na mfumo wa dini hiyo ili awafundishe vizuri wanafunzi wake ambao walikuwa tayari kukubali mafundisho safi. E.G. White anasema:" Hitherto He had called the temple His Father's house; but now, as the Son of God should pass out from those walls, God's presence would be withdrawn forever from the temple built to His glory. Henceforth its ceremonies would be meaningless, its services a mockery. {DA 620.4}Hatimaye Yesu na wanafunzi wake walijitenga na hekalu lililokuwa mpendwa wao. Lakini kwa sababu viongozi wa hekalu walikataa kufuata mafundisho ya neno la Mungu peke yake, Mwana wa Mungu hakuona sababu ya kuendelea kubaki ndani ya hekalu ingawa “Alikuwa akiliita hekalu kuwa ni nyumba ya Baba yake; lakini sasa, kama Mwana wa Mungu ambavyo akipita kutoka katika kuta hizo, uwepo wa Mungu ungeondolewa milele usionekane ndani ya hekalu lililojengwa kwa utukufu Wake. Hivyo sherehe zilizofanyika ndani ya hekalu hazikuwa na maana, huduma zake zikawa dhihaka”. {DA 620.4}. Hivyo ndivyo alivyofanya Martin Luther na wafuasi wake.

Baada ya kifo cha Martin Luther, wafuasi wake waliendelea katika kufanya matengenezo. Hata hivyo kwa sababu freemasons hawakati tamaa, matengenezo yalikoma na kuanza kurudi nyuma taratibu ambapo leo hii wale wanaoitwa ‘Walutheri’ wameungana tena na mfumo ambao mwanzilishi wao, Martin Luther, aliuiita ‘mfumo mchafu’.

Wakati matengenezo yanaendelea, ulikuwa ni wakati wa kutimizwa kwa unabii wa siku 1260 sawa na miaka 1260 kama ilivyotabiriwa na nabii Yohana. Wakati huo kulianzishwa matengenezo mengi na kupelekea kuanzishwa kwa mifumo mingine ya makanisa. Baadhi ya makanisa yaliyoanzishwa yalikuwa haya:

Anglican: Lilianzishwa huko England na mfalme wa Uingereza ili kupinga kanisa la Roma. Kiongozi mkuu wa kanisa hilo ni Malkia wa Uingereza. Hata hivyo wachunguzi wa dini ya freemasons wanasema kwamba familia ya Malkia ni familia mojawapo kati ya familia 13 za waumini wa Freemasons.

Presbyterian: Mwanzilishi ni John Calvin mwaka 1509 – 1564 na John Knox 1505 – 1572. Kanisa hili lilijitenga na Roma likiwa na motto “Chunguza maandiko” maana liliona kwamba kanisa la Roma linakwenda kinyume na maandiko. Hata hivyo wafuasi wa John Calvin na John Knox wameshindwa kufikia malengo ya kuyachunguza maandiko na kufuata kile asemacho Mungu na badala yake wamekubali kurudi walikotoka!

MENNONITE: Lilizaliwa rasmi mwaka 1525 – 1530 na Conrad Grebel na wenzake akiwemo Zwingli Ulrich aliyetofautiana na Martin Luther juu ya somo la pasaka. Hawa walikataa ubatizo wa Roma wa kunyunyizia maji na jina jingine wanaitwa “Meno Knights” majina ambayo yanafanana na vikundi vya Freemason kama vile “The knights of Eulogia”(Skull and Bones), “The knights of Malta”. Ingawa lengo la Zwingli Ulrich lilikuwa zuri, baada ya kifo chake wafuasi wake walikubali kuingiliwa na freemasons na hivyo kushindwa kufikia lengo lililokusudiwa.

LUTHERAN: Mwanzilishi ni Martin Luther mwaka 1517. Alikuwa ni Mjerumani aliyesomea ukasisi wa kanisa la Roma na mwaka 1511 akapata Phd katika chuo kikuu cha Wattenberg. Alipingana na kanisa lake la Roma na kuandika sababu 95 zinazopinga mafundisho ya Roma ndipo akajitenga na Roma na hivyo wafuasi wake wakaendelea kutumia jina la Lutheran, yaani wafuasi wa Luther. Wafuasi wa Luther hawakuendelea mbele na sasa wamerudi kwenye makosa aliyokuwa akiyapinga Luther. Je, Lutheran wa leo wanafuata kweli nyayo za Martin Luther? Au wametekwa kwa matumizi ya njama ya “Following Gurus”yaani kufuata kila wasemacho viongozi? Tafakari!

Moravian: Mwanzilishi ni John Huss aliyezaliwa mwaka 1366 na kuchomwa moto na papa hadi kufa mwaka 1416 baada ya kulipinga kanisa la Roma. Wafuasi wake hadi leo wanaitwa kanisa la Moravian. Kwa bahati mbaya wafuasi wa John Huss hawakuendelea kufanya matengezo ili kusonga mbele zaidi ya Huss na kibaya zaidi ni kwamba wanarudi nyuma badala ya kusonga mbele. Leo Huss akifufuka atashangaa kuona jinsi wafuasi wake walivyoacha kanuni alizozianzisha. Je, wamoravian wa leo wako tayari kuchomwa moto kwa kutetea ukweli kama John Huss? Tafakari!

Baptist: Ni kanisa lililoanzishwa na wafuasi wa Martin Luther ambao walijitenga na Lutheran mwaka 1600 huko Uholanzi na Uingereza baada ya kuona kwamba wafuasi wenzao wameacha kanuni alizoziweka Martin Luther. Hata hivyo kanisa la Baptist la leo haliendeleza jitihada za Luther na sasa badala ya kusonga mbele linapiga ‘marktime’ likiwa limegeuka nyuma.

Salvation Army (Jeshi la Wokovu): Mwanzilishi ni Booth mwaka 1878. Kanisa hili lilianzishwa na wafuasi wa freemasons kwa lengo la kuchafua matengenezo ya kweli. Kumbuka kwamba Shetani hutumia fursa inayotolewa na Mungu akiwa na lengo la kuwafanya watu washindwe kujua kipi ni cha kweli na kipi sio. Katika kila matengenezo ya kweli, pamekuwepo na matengenezo bandia.

Marmon church: Mwanzilishi ni Joseph Smith (1805 – 1844). Kanisa hili linajulikana pia kama The church of Jesus Christ of later day saints. Kanisa la Mormon lilianzishwa na wafuasi wa freemason wakiwa na lengo la kuchafua matengenezo ya kweli. Mitt Romney ni muumini wa kanisa la Mormon.

Methodist: Kiongozi Mwanzilishi ni John Wesley. Lilianzishwa na watu 17 wa familia moja mwaka 1738 likiwa na lengo la kupinga mafundisho ya freemasons. Kanisa hilo halijakamilisha lengo la matengenezo kutokana na ukweli kwamba wafuasi wake hawana mwamko aliokuwa nao John Wesley.

Watch Tower: Mwanzilishi ni Charles T. Russel 1852 – 1916 na mwenzake J. Lutheford 1869 – 1942. Baba yake Charles T. Russel alikuwa ni mchungaji wa Prebyterian. Mnamo mwaka 1932 huko Marekani jina la kanisa hilo lilibadilishwa na kuitwa Mashahidi wa Yehova. Markus Mpangala ameelezea kwa kirefu chanzo cha dhehebu hili akiainisha kwamba waanzilishi walikuwa ni Freemasons kutoka kwenye familia ya Illuminati inayoitwa Russel illuminati bloodline ambayo nimeshaielezea kwenye makala zilizopita.

Brethen Assemblies: Mwanzilishi ni ndg. Dabi 1800 – 1882 ambaye alikuwa ni muumini wa Anglican na akajitenga na kanisa hilo na kuanzisha kanisa lake. Dabi aliamua kujitenga na Anglican kutokana na kanisa hilo kutawaliwa na familia ya freemasons.

Makanisa ya Kipentekoste au kilokole: Ni makanisa yaliyoanzishwa miaka ya hivi karibuni. Makanisa haya yalianzishwa huko Kansas City Marekani mwaka 1901kwa lengo la kupata nguvu ya kile kinachoaminiwa kuwa roho mtakatifu. Je, unajua uhusiano uliopo kati ya muziki wa‘rap’ au ‘kufoka’ na uvuvio wa kunena kwa lugha kutoka kwa kile kinachoaminiwa kuwa ni nguvu za roho mtakatifu wakati waumini wa kilokole wanapokuwa wakiomba? Kumbuka kwamba Muziki wa rap ulianzia huko Kansas City Marekani, mahali ambako makanisa ya kipentekoste yalianzishwa. Panapo majaaliwa, nitakuwa na makala ndefu kuhusu asili, lengo na nguvu inayoonekana kwa viongozi wa makanisa ya kilokole kama akina T.B Joshua wa SCOAN la huko Nigeria. Kwa wakati huu nasema,‘Soma Biblia na Tafakari’!

Gospel terbenacle: Mwanzilishi ni Pastor A.B. Simpson mwaka 1881 akitokea Presybiterian.

Christian Churches: Mwanzilishi ni Thomas Chapel mwaka 1807 akitokea Presybiterian.

Seventh –Day Advetist Church: Mwaka 1844 baada ya kutokurejea kwa Yesu duniani kama ilivyohubiriwa na muhubiri mashuhuri aitwaye William Miller, watu wengi walivunjika moyo isipokuwa watu 50 tu ndio walioendelea kujifunza Biblia miongoni mwao akiwa ni Ellen G. White. Watu hao waliendelea kuchunguza makosa yaliyofanywa na William Miller maana wao pia waliamini juu ya marejeo ya Yesu tarehe 22/10/1844. Hatimaye mwaka 1863 kanisa hilo likapewa jina la Seventh –Day Adventists Church huku likiwa na motto au kauli mbiu ya “Amri za Mungu na imani ya Yesu na Ujumbe wa malaika watatu” na baadaye kanisa hilo likawa chini ya rais wa General Conference ya SDA makao makuu yake yakiwa huko Marekani. Rais huyo ndiye kiongozi (kichwa) mkuu wa kanisa hilo duniani na huchaguliwa kila baada ya miaka mitano. Wakati viongozi wa kanisa walipokutana ili kujadili mambo ya kanisa, palikuwa na ‘Mwenyekiti’(Chairman of General Conference) ambaye aliongoza kikao hadi mwisho. Baada ya kikao kumalizika, mwenyekiti huyo alimaliza muda na kazi yake. Hata hivyo kulitokea mabadiliko kutokamwenyekiti wa baraza kuu hadi na rais wa kanisa ulimwenguni. Kila baada ya miaka mitano hufanyika uchaguzi wa kumpata rais wa kanisa hilo. Tofauti na makanisa mengine, kanisa hili linaabudu siku ya Jumamosi wakati makanisa mengine yanaabudu siku ya jumapili. Sasa hivi kuna makanisa mengi ya SDA ambayo yametoka ndani ya kanisa la ‘General conference of Seventh-Day Adventists’(GCSDA) kwa madai kwamba kanisa hilo limeingiliwa na freemasons. Wengi wa waumini wa SDA waliojitenga na GCSDA wanasema kwamba walikuwa wakipinga‘protest’ mafundisho machafu huku wakiendelea kuwa ndani ya GCSDA lakini hawakuweza kuleta mabadiliko yoyote maana hali ilikuwa inazidi kuwa mbaya. Hatimaye waumini hao waliamua kufuata nyayo za akina Luther za kujitenga na sasa wanafanya ‘reformation’ au ‘matengenezo’ hatua kwa hatua maana walitoka na mafundisho machafu ambayo waliyapokea kama kweli wakiwa ndani ya GCSDA.Waumini hao wanadai kwamba walijitenga na GCSDA kwa sababu



Je, madai hayo ni kweli? Tafakari!

Msingi wa kanisa la SDA au ‘Wasabato’ kama inavyojulikana kwa wengi,kuabudu siku ya jumamosi, ni kile kilichoandikwa na Mungu wakati wa uumbaji, kwamba aliumba kwa siku 6 na siku ya 7 akastarehe, akaibariki na akapumzika kisha akawaambia waisraeli: “Ikumbuke siku ya Sabatouitakase….” Kutoka 20:8.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname