Trafiki akimdhibiti dereva wa gari dogo aina ya Toyota Pick up.
SEKESEKE la
aina yake kati ya dereva wa gari dogo aina ya Toyota Pick up na trafiki
ambao majina yao hayakujulikana mara moja liliibuka na kuzua maswali
mengi kwa mashuhuda huku mambo ya rushwa yakitajwatajwa. Tukio hilo lilizozua maswali mengi liliibuka juzi Jumatano, Bamaga, Mwenge jijini Dar jirani na kituo cha mafuta cha Bamaga.
Katika tukio
hilo, dereva huyo na trafiki walikuwa wakikunjana, ambapo dereva alikuwa
akilalamika kuonewa (Haikujulikana kivipi) wakati askari huyo wa
usalama barabarani akisisitiza kuwa jamaa huyo alivunja sheria.
Gari aina ya 'Land Rover' (break down) lililotumika kuvuta gari la aina ya Toyota Pick up la dereva huyo.
ILIKUWAJE?
Kikosi cha
Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ cha Global Publishers, kikiwa katika
pitapita zake za kusaka matukio na kuhakikisha maadili hayavunjwi ndipo
kilipokutana na kisanga hicho cha kushangaza.
Trafiki alisikika akimwambia
dereva kuwa amevunja sheria za barabarani huku gari lake likiwa bovu
hivyo aliamuru gari hilo kuvutwa hadi kituoni kwa ajili ya ukaguzi
lakini dereva huyo alikataa.
...ilikuwa ni vigumu sana kwa dereva huyo kukubali gari lake kukamatwa.
DEREVA
Pamoja na
kuelezwa kuwa gari lake lilikuwa na matatizo na mahali alipoegesha
hapakuwa sahihi, dereva huyo alipayuka: “Nawajua nyie trafiki, kazi yenu
ni kuonea watu sasa mimi sitoi kitu hapa, labda mniue.“Siendi popote,
mkiondoa gari nalala mbele yake ili mnigonge nife, mimi nimesema
silitoi.”
...dereva akizidi kubisha kwa uamuzi uliochukuliwa na afisa usalama wa barabarani 'trafiki' .
TRAFIKI
Trafiki
huyo aliyeonekana kuwa makini na kazi yake, hakuwa na makuu, zaidi
alitaka gari livutwe hadi kituoni huko sheria ingefuata mkondo wake
baada ya ukaguzi.
Mashuhuda wa tukio hilo,
waliliambia Ijumaa kuwa, kilichohitajika ilikuwa ni busara ya
masikilizano kuliko kuvutana kwa maneno na afisa wa polisi.
Afisa usalama wa barabarani akisisitiza kulichukua gari la dereva huyo kwa ukaguzi zaidi.
“Sasa
kama gari lake anajua ni zima, anabishana nini na polisi? Ikiwa
anajiamini kuwa aliegesha sehemu sahihi, hofu yake ni nini? Kama kweli
anajua yupo sawa, anatakiwa kukubali kwenda polisi, gari likakaguliwe.
“Wakati mwingine unaweza
kuwalaumu tu askari, kumbe ni tabia ya watu kukataa kutii sheria bila
shuruti. Sasa anafikiri kwa maneno makali anayotoa kwa huyo askari
atamwachia?
Raia wakishuhudia mkasa huo uliotokea katika kituo cha mabasi yaendayo Mwenge cha Bamaga.
“Anasema
eti hatoi kitu, kwani kaombw TWENZETa rushwa pale au anadhani kila
trafiki anayemkamata dereva aliyevunja sheria anataka rushwa?” alisikika
shuhuda mmoja akihoji kwa jazba.
Hata hivyo,
pamoja na mkwara wa jamaa huyo, gari lake lilifanikiwa kuvutwa kuelekea
polisi ambapo jamaa huyo alipanda gari lingine kulifuata.
No comments:
Post a Comment