Hisia:
Neymar alimwaga machozi, huku akiweka wazi kuwa alikaribia kuwa kichaa
baada ya Juan Zuniga kumfanyia faulo mbaya kwenye mchezo wa robo fainali
ya kombe la dunia dhidi ya Colombia.
NYOTA
wa Brazil, Neymar Jr amefichua siri kuwa alishindwa kuzuia machozi na
alikaribia kuwa kichaa baada ya kugongwa na Juan Zuniga na kuvunjika
mfupa wa uti wa mgongo.
Neymar
kwa mara ya kwanza alifanya mkutano na waandishi wa habari baada ya
kutoka Hospitalini ambapo anauguza majeraha yake ya mfupa wa uti wa
mgongo uliovunjika kwenye mechi ya robo fainali ya kombe la dunia dhidi
ya Colombia.
Pia
Neymar hajakubaliana na maneno ya wakala wake aliyemuita Luiz Felipe
Scolari kuwa ni kocha mbaya, mwenye majivuno na aliyepitwa na wakati.
Hii
inatokana na kitendo cha Brazil kufungwa mabao 7-1 dhidi ya Ujerumani
katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la dunia, jumanne ya wiki hii.
Mshambuliaji
huyo mwenye miaka 22 ameweka wazi kuwa beki wa Colombia, Juan Zuniga
ambaye alimgonga na goti kwenye uti wa mgongo alimpigia simu na kuomba
radhi kwa kitendo hicho kilichomfanya asicheze tena michuano hii mikubwa
duniani.
Neymar jana alitembelea kambi ya mazoezi ya timu ya Taifa ya Brazil iliyopo mjini Teresopolis na aliwasalimia wachezaji wenzake.
Pia ataambatana na wenzake hapo kesho katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu dhidi ya timu ya taifa ya Uholanzi.
Jumapili katika dimba la Maracana, mjini Rio di Janeiro, Argentina itacheza mechi ya fainali dhidi ya Ujerumani.
Machozi: Neymar alishindwa kuendelea kucheza fainali za kombe la dunia baada ya kuvunjika mfupa wa uti wa mgongo.
Kwaheri: Neymar aliweza kutabasamu wakati akiondoka kwenye mkutano wa kwanza na waandishi wa Brazil tangu apate majeruhi.
Amani:
Neymar alikiri kuwa Zuniga amempigia simu na kumuomba radhi kwa kitendo
alichomfanyia na kumaliza ndoto zake za kucheza kombe la dunia
No comments:
Post a Comment