07 July 2014

RUBANI AVUA NGUO MBELE YA ABIRIA WAKE



Rubani wa shirika la ndege ya Afrika Kusini, South African Airways amekamatwa na askari wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Harare baada ya kuvua nguo zake zote mbele ya abiria na wahudumu wengine wa ndege hiyo na kubaki na nguo ya ndani.
Rubani huyo, W Van Ginkel ambaye alikuwa airushe ndege yenye namba SA 025 kutoka Harare Zimbabwe kuelekea Johannesburg Afrika Kusini, alifikia uamuzi wa kuvua nguo zake wakati akipita katika eneo la kukaguliwa abiria, ambapo Baada ya kukaguliwa, akiwa anataka kuondoka kifaa cha ukaguzi kikatoa mlio, ambapo aliamriwa kuvua viatu.
Hata baada ya kuvua viatu, kifaa hicho kiliendelea kutoa mlio kila akipita eneo la ukaguzi, ambapo aliamriwa kutoa mkanda wa suruali yake na alipofanya hivyo kifaa hicho kiliendelea kutoa mlio hali iliyomkera rubani huyo na kuamua kuvua nguzo zake zote na kubaki na nguo ya ndani, hali iliyowalazimu polisi kumkamata.
Kufauatia tukio hilo, zaidi ya abiria 90 waliokuwa wasafiri na ndege hiyo walilazimika kusubiri kwa saa tano hadi pale alipopelekwa rubani mwingine

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname