18 July 2014

MONALISA AMSAPRAIZI BABA' AKE...KIVIPI?! FUATILIA ZAIDI HAPA

Staa wa filamu za Kibongo, Yvonne Sheryl  ‘Monalisa’ akilishwa keki na baba yake mzee Alex Humba
Staa wa filamu za Kibongo, Yvonne Sheryl  ‘Monalisa’ juzi kati alimfanyia sapraizi ya kumpelekea keki baba yake wa kufikia Alex Humba Lumila ambaye ni mume wa mama yake Suzan Lewis ‘Natasha’ katika siku yake ya kuzaliwa.Staa huyo alifanya kisherehe hicho cha kushitukiza kilichochukua nusu saa ikiwa ni katika kuonesha upendo wake kwake, hali iliyomfanya mzee Humba abaki amepigwa na butwaa huku akionesha furaha aliyokuwa nayo.
Mzee Alex Humba akimlisha keki mkewe Suzan Lewis ‘Natasha’. 
 Akizungumzia tukio hilo, mama wa Mona, Natasha alisema: “Nimefurahi sana, namshukuru mtoto wangu Mona kwani sikutarajia kama atamfanyia baba yake sherehe hii kwani hata mimi alinificha ila imeleta upendo mkubwa ndani ya nyumba kama hivi unavyoona tunasherehekea.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname