Hata
kama utapingana na mimi, lakini ukweli utabaki pale pale; Kila jinsia
inahitaji sana kuungana na jinsia nyingine katika tendo muhimu na la
kihistoria katika maisha liitwalo ndoa! Yes, huu ni ukweli ambao upo
wazi na utaendelea kusimama kama ulivyo.
anasubiri kufuatwa na mwanaume,
wakati mwanaume anaamua kumfuata mwanamke anayemtaka na kwa wakati wake.
Kuna kitu nataka kuweka sawa hapa, kwamba wanaume
ndiyo huwa wa kwanza kupenda kabla ya mwanamke, ingawa mwanamke anaweza kuwa wa kwanza kupenda lakini akashindwa kufikisha hisia zake kwa mwanaume husika.
ndiyo huwa wa kwanza kupenda kabla ya mwanamke, ingawa mwanamke anaweza kuwa wa kwanza kupenda lakini akashindwa kufikisha hisia zake kwa mwanaume husika.
Wanawake wa ‘mjini’ huwa
hawakubaliani na hili, kutokana na huu utandawazi unaohubiriwa siku hizi
ikiwa ni pamoja na kampeni za usawa zinazotetewa na Wanaharakati
Wanawake. Akina dada nao huchangamkia kueleza hisia zao kwa wanaume.
Nadhani si jambo baya, ingawa linaweza kupokelewa kwa hisia tofauti na
kila mwanaume.
Tuyaache hayo, hoja kubwa ya msingi
hapa ni jinsi gani mwanamke anaweza kuolewa haraka na mpenzi wake.
Ikumbukwe kwamba, hapa nazungumza na wanawake ambao tayari wapo katika
uhusiano, lakini wenzi wao hawana habari kabisa na mambo ya ndoa.
Katika matoleo yaliyopita, niliwahi
kuzungumza kuhusu namna gani mwanamke anaweza kuwashawishi wanaume
wakataka kuingia katika uhusiano naye. Leo nazungumzia juu ya wewe
ambaye upo katika uhusiano ambao haueleweki, lakini ndoa unaitaka.
Unajua cha kufanya? Fuatana nami.
EPUKA MAKUNDI HATARI
Mwanaume anapenda kuwa na mke mwenye
staha, ambaye hana tabia za hovyo. Kuwa na makundi ya ‘mashangingi’ ni
alama ya kwanza kabisa kuwa unapenda au tayari una tabia za kishangingi.
Wanaume wengi hawapendi kabisa wanawake wenye tabia za hovyo, wenye
kampani ambazo si nzuri.
Lakini yawezekana, jamaa
alishakuambia juu ya kilio chake hiki, lakini wewe umekuwa kama umeweka
pamba masikioni mwako, hili ni tatizo. Linda heshima yako, kaa mbali na
makundi hatari, ili umfanye jamaa akuone wewe ni mwanamke thabiti ambaye
huigi, hushabikii na wala huna tabia mbaya. Utaonesha hili kwa kukaa
mbali na makundi ya wanawake hatari! Umenipata?
ZINGATIA MAVAZI YAKO
Kila mtu anamjua mtu wake alivyo,
mwanamke hata wewe unamjua mpenzi wako alivyo. Sina shaka unafahamu
anapenda nini na nini anachukia. Unajua kabisa, nina uhakika na hilo.
Lakini pamoja na kwamba jamaa anaweza kuwa na vitu ambavyo vinamvutia
zaidi, hata wewe kama mtoto wa kike, una mapendekezo yako au vitu
ambavyo unapenda zaidi kuvifanya!
Huzuiwi, lakini swali la msingi,
mwenzi wako anapenda? Kama wewe unapenda sana skin jeans na top
inayoacha kitovu nje, yeye hapendi kwa sababu ana nia ya kukufanya mke
hapo baadaye. Sasa utakuwa mke gani ambaye hata Salim anaona sehemu zako
za faragha hadharani?
Ukiachana na chaguo la mwenzi wako,
lakini lazima wewe mwenyewe kama mwanamke wa mtu, ujitambue! Jisitiri
vyema. Kwani kuna urembo gani wa kuvaa nguo inayoonesha mwili wako
ulivyo? Kuna burudani gani kuacha nyeti zako wazi? Unataka nani akuone
ulivyo? Mke hana sifa hiyo dada yangu, sasa ili uweze kuwa na sifa hii
muhimu, lazima uzingatie sana mavazi yako.
JIPE MOYO
Hili nilishawahi kulizungumza sana
katika mada zilizopita, baadhi ya wanawake wamekuwa wakikatishwa tamaa
na rafiki zao au watu wengine wanaowazunguka, eti hawana hadhi ya
kuolewa au watahangaika sana lakini hawatapata mume, kisa eti HAVUTII!
Mwingine anajinyima mwenyewe nafasi
akisema; “Mimi nina balaa, sina bahati ya kuolewa, ndiyo maana wadogo
zangu wote wameolewa nimebaki mimi.”
Huu ni uvivu wa kuwaza. Lakini dada yangu, habari iliyo njema kwako ni kwamba, ndoa unaitengeneza wewe mwenyewe.
Unaitengeneza kwa misingi ya kwanza,
kujipa moyo mwenyewe kwamba wewe ni mzuri na una sifa na haki za
kuolewa kama wanawake wengine. Jipe moyo mwenyewe, huna nuksi wala
balaa, wewe ni mzuri na una sifa za kuwa mke hapo baadaye.
Iko hivi, ukianza kujishusha
mwenyewe, ni dhahiri kwamba hata mavazi yako hayatakuwa mazuri, uso wako
hautakuwa na tabasamu na wala hutakuwa na matumani moyoni, hapo sasa ni
mwanzo wa kuzorota afya yako. Utapata mchumba kweli? Utasubiri sana kwa
mtindo huo.
ACHA PAPARA
Haizuiwi kuuliza kuhusu mustakabali
wa uchumba wenu, lakini ni vizuri basi kuwa na kiasi. Kuuliza kila
wakati au kuwa mtu wa kulaumu, hakutakusaidia kumfanya jamaa achukue
maamuzi ya haraka ya kukuoa na badala yake yanaweza kumpa picha tofauti.
Ni rahisi kuwaza kwamba,
unachohitaji kwake ni ndoa na baada ya hapo hutakuwa na staha tena. Kuwa
mjanja, achana na papara. Usilogwe ukamfanyia jambo zuri mpenzi wako,
halafu ndiyo umuulize; “Sasa honey, mbona hata huzungumzii ndoa yetu?
Hivi utanioa kweli? Eeeh baby? Niambie basi mpenzi wangu.
No comments:
Post a Comment