28 July 2014

"..JAMANI NGOJA NIMNYONYESHE MWANANGU MAANA BADO MDOGO NA MIMI NI...." FLORA MVUNGI WA BONGO MOVIE AFUNGUKA KUHUSU UKOBE!

Staa wa filamu za Kibongo, Flora Mvungi.
FUNGUKA! Staa wa filamu za Kibongo, Flora Mvungi ambaye ni mke wa ndoa wa msanii wa muziki wa Kizazi Kipya, Hamis Ramadhan ‘H. Baba’ amefunguka kwamba mwaka huu ameshindwa kufunga Mwezi Mtukufu (ukobe) kwa sababu ananyonyesha.

Akijibu minong’ono ya watu iliyohoji kwa nini hafungi, Flora alisema kutokana na mwanaye kuwa mchanga na kila mara anataka kunyonya, ameshindwa kufunga kwani imekuwa vigumu kutokana na kupatwa na njaa ya mara kwa mara. “Jamani ngoja tu nimnyonyeshe mwanangu maana bado mdogo na mimi ni mzazi hivyo sikuweza kufunga, ninatakiwa nile kila wakati kwa sababu mwanangu ananyonya sana, msinitafsiri vibaya,” alisema Flora ambaye amekuwa kibonge kupindukia.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname