Nyota wa sinema za Kibongo, Irene Uwoya amefunguka juu ya tuhuma za kufanya fujo nyumbani kwa mume wa mtu zilizoripotiwa na mitandao mbalimbali ya habari nchini hivi karibuni.
Akizungumza exclusively
nasi, Irene amesema kuwa haelewi hizo tuhuma zimetoka wapi na wala
hajui aanzie wapi kuzijibu maana siyo yote yaliyoripotiwa ni kweli.
Tuhuma
hizo zilidai kuwa, mwanadada huyo mrembo alienda kuleta timbwili
nyumbani kwa mume wa mtu huyo baada ya kusikia kuwa jamaa huyoa ameamua
kuoa na kumoiga chini Irene aliyekuwa akitoka naye kipindi cha nyuma.
“Uwoya alitegemea angeolewa yeye, sasa kusikia jamaa kaoa mwanamke mwingine tena kwa siri, ilimfanya aishiwe nguvu,” Habari hizo ziliriripoti.
Habari
zinazidi kudai kwamba, alichoamini Uwoya ni kwamba kitendo cha mwanaume
huyo kuoa kingemfanya yeye aendelee kuwa ‘nyumba ndogo’ jambo ambalo
hakupenda kulisikia hata kidogo.
Akifafanua tukio hilo Zaidi uwoya alisema.
“Ilitokea, lakini nilishaachana naye. Unajua ishu si kwamba angenioa mimi, ila kitendo alichokifanya hakikuwa cha uungwana,” alisema Uwoya.
No comments:
Post a Comment