Mchekeshaji
wa kundi la Orijino Komedi, Emmanuel Mgaya maarufu kama Masanja
Mkandamizaji’ amesema yupo kwenye mipango na maandalizi ya kufunga ndoa
kabla mwaka huu haujamalizika.
Akizungumza
na kituo cha redio cha Praise Power, leo, Masanja amesema kuna
maandalizi ambayo anayafanya ili kukamilisha mchakato huo.
“Namwamini
Mungu huu mwaka hauzami,” alisema. “Pale kitandani tutakuwa tunalala
wawili na katika kitu nimekimisi nafikiri ni ile kamba ya kuanikia nguo
nyumbani, itakuwa hata inanilaumu, haina hata nguo mchanganyiko.
Inapendeza unapita pale nyumbani kwetu unaona pale tumeanika kasuruali,
kanga, sketi. Natamani ile kamba yangu ya nguo ifanye vitu mchanganyiko,
lakini ninamwamini Mungu, mwaka huu mwishoni mwishoni ukipita nyumbani
utakuta kamba ina mchanganyiko wa nguo,” aliongeza.
No comments:
Post a Comment