17 July 2014

INASIKITISHA SANA: UKATILI WA KUTISHA..HIVI NDIVYO BOSI ALIVYONUSURIKA KUUAWA KWA RISASI NA MAPANGA TABORA

 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, Geita, Juma Kimisha akiwa Hospitali ya Wilaya ya Kahama Kitengo cha Bima.
 Watu wasiojulikana wamemshambulia kwa risasi na mapanga Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, Geita, Juma Kimisha na msafara wake na kusababisha kiongozi huyo kukimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza ili kuokoa uhai wake.Akizungumza kwa shida katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama Kitengo cha Bima ambapo alipatiwa huduma za matibabu kwa lengo la kuokoa uhai wake kabla ya kupewa rufaa ya matibabu kwenda Bugando jijini Mwanza, Kimisha alisema mbali ya kujeruhiwa waliibiwa mali zao. Alisema tukio hilo lilitokea Julai 3, 2014, saa mbili na nusu usiku katika Kata ya Igusule wilayani Nzega wakiwa hatua chache kufika katika mpaka wa Mikoa ya Tabora na Shinyanga, walipokuwa wakitoka jijini Tanga katika maadhimisho ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAAT). 
Mwenyekiti huyo alisema akiwa katika gari la Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu lenye namba za Usajili SM 10032 (pichani) lililokuwa likiendeshwa na Joseph Dutu Machibya, walikuta kizuizi cha mawe makubwa barabarani katika eneo walilotekwa na kuwalazimu kusimama ndipo waliposhtukia mvua za risasi zikilisakama gari lao.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname