Nadhani ulishawahi kusikia ama
kushuhudia watu wa eneo Fulani ama jamii fulani wakimlazimisha kichaa
kuoga kwa nguvu kwa kuwa amezidi kuwa mchafu, lakini hii ni tofauti kwa
waumini wa dhehebu analolisimamia mchungaji Wale Olanguji wa Nigeria.Mchungaji
Wale wa kanisa la Divine Seed of God wa Ibadan, Oyo, Nigeria ameliambia
jarida la People City la Nigeria kuwa hajawahi kuoga tangu mwaka 2001
wakati ambapo anadai alipokea amri ya Mungu ikimtaka afanye hivyo na
kwamba ajitenge na mkewe na kuacha kutumia baadhi ya vinywaji.
Cha ajabu, licha ya kukaa miaka 13 bila kuoga mchungaji huyo hatoi
harufu na ni vigumu kumshitukia hadi akuoneshe mwenyewe vielelezo!
Hivi ndivyo mchungaji huyo alivyoliambia jarida hilo wakati
lilipomkumbusha kuwa mwaka 2001 alitoa maelezo kuwa Mungu amemwambia
asioge:
"Ndiyo, ni miaka 13 hadi sasa kwa ufupi. Mwaka 2000 mwanzoni Mungu
aliniambia niache kuoga, nijitenge na mke wangu na kwamba natakiwa
kuacha kutumia vinywaji vyote laini pamoja na wines. Na tangu wakati
huo…kwa kweli, nimekuwa nikifuata yote hayo.
"Mtu yeyote ambaye Mungu anataka kumtumia kwa sababu hapa duniani, kuna
gharama imeambatanishwa kwenye huo wito. Kwa hiyo ninaamini kwamba hiyo
ni gharama ninayolipa. Ninavyoongea na wewe hivi sasa, sijaoga, kama
unataka nikuoneshe ushahidi nitakuonesha kama una shaka juu ya haya yote
nisemayo; sijaoga tangu mwaka 2001 hadi wakati huu."
No comments:
Post a Comment