Kampuni moja ya kitaliii kutoka nchini China
imesema kuwa itawashtaki watengenezaji wa filamu mpya ya Transformers
kwa kuvunja mkataba.
Kampuni ya Chongqing Wulong Karst Tourism Co Ltd imesema katika
taarifa yake kuwa watengenezaji wa filamu hiyo wameshindwa kuonyesha
lebo yao vizuri katika filamu hiyo kama walivyoahidi.
Wanasema itafungua kesi dhidi ya kampuni ya Paramount Pictures na moja ya washirika wake kampuni kutoka China.
Paramount bado haijasema chochote mpaka sasa kuhusiana na madai hayo
No comments:
Post a Comment