STAA wa
filamu za Kibongo, Kajala Masanja ameibuka na kusema kuwa ushosti wake
na Miss Tanzania 2006/07, Wema Sepetu, uliorudishwa hivi karibuni baada
ya kuwekana sawa ni wa kinafiki huku akidai Wema ni kigeugeu.
Staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja
Akizungumza kwa kujiamini mbele ya waandishi wetu, juzi Jumatano pande
wa Mikocheni jijini Dar es Salaam, Kajala alisema: “Wema ni mnafiki
kabisa. Upatanisho wetu ni wa uongo. Mimi moyoni nimeondoa kinyongo
lakini mwenzangu naona kama bado ana donge moyoni.”
Kajala alisema hayo alipoulizwa na Risasi Jumamosi, sababu ya
kutoonekana kwenye tukio la futari lililofanyika nyumbani kwa mama mzazi
wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ambaye ni mkwe
wa shosti wake huyo.
Katika tukio hilo, mama Diamond alifanyiwa sapraizi ya nguvu
alipokabidhiwa gari kali aina ya Toyota Lexus Harrier kama zawadi ya
bethidei yake, ambayo ilitolewa na meneja wa Diamond, Babu Tale kwa
niaba ya mwanamuziki huyo ambaye alikuwa safarini nchini Marekani.
Miss Tanzania 2006/07, Wema Sepetu,
“Tunakubaliana kuwa kitu kimoja lakini mwenzangu anaonekana ana
kinyongo. Hebu angalia, anawezaje kuacha kunialika kwenye shughuli
muhimu kama ile kama kweli tumepatana? Mbona amealika watu wengi lakini
mimi ameniacha? Wema aache unafiki bwana.
“Mbaya zaidi, hivi juzi tu ameweka picha ya msichana mmoja anayekaa
China, huyu mdada anaitwa Sabrina, niliwahi kugomabana naye, lakini yeye
amemuweka Instagram na kumwandikia maneno kibao ya kumsifia akim-wish
happy birthday, hapo si kama ananisimanga? Wema si mkweli,” alisema
Kajala.
Akizungumzia ishu hiyo, siku ya tukio Wema alisema: “Ukiniuliza kuhusu
Kajala kutokuwepo hapa, kwa kweli utakuwa kama unanichanganya tu maana
leo sijashika simu muda mrefu sana.
“Hata ujio wangu hapa nilikurupushwa, ndiyo maana sijakumbuka kumuita
Kajala, lakini tuko vizuri na mara ya mwisho tumeongea jana (Jumapili)
usiku tu,” alisema Wema
No comments:
Post a Comment