kijana Peter Sitiwati akiwa na maumivu makali yaliyosababishwa na kuoza kwa mguu.
AMA kweli ng’ombe wa maskini hazai, kijana Peter Sitiwati (26), mkazi wa Sinza ya kwa Remmy jijini Dar amejikuta akikatisha ndoto za utafutaji maisha kufuatia kuoza mguu baada ya ajali mbaya ya gari.Akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar juzi kati kwa sauti ya kukata tamaa, Peter alisema alipata ajali ya gari mwaka 2013 maeneo ya Sinza-Mori, Dar na kuumia vibaya mguu wa kulia.’’Baada ya kugongwa na gari niliangukia mtaroni nikachomwa na kijiti kwenye mguu wa kulia. Nilikimbizwa Hospitali ya Palestina kutibiwa na baada ya muda mguu ulionesha kupona kwa juu, lakini kumbe ndani kidonda kilikuwa kibichi na kiliendelea kulika bila mimi kujua.
“Mwanzoni mwa mwaka huu (2014) nikaanza kushangaa usaha mwingi unatoka sehemu mbalimbali ya mguu tena na harufu mbaya, mguu ukaonekana umeoza tena una matundu matatu, si unauona ulivyo, hata watu hawapendi kukaa jirani na mimi,” alisema Peter huku akionesha mguu wake huo.endelea >>>>>>>>>>>>.
No comments:
Post a Comment