Gari
lenye namba IT 7945 Toyota Nadia likiendeshwa na EDSON MWAKABUNGU (31)
mkazi wa Tabata Dar es Salaam liliacha njia na kugonga gema na
kusababisha majeraha kwa watu watatu baada ya kugongwa na gari jingine
linalosadikiwa kuwa Fuso.Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi David
Misime SACP amesema ajali hiyo imetokea tarehe 26.07.2014 saa tisa
alfajiri katika barabara kuu ya Morogoro – Dodoma eneo la Ranch ya NARCO
Wilaya ya Kongwa.
Waliojeruhiwa
ni EDSON MWAKABUNGU ambae analalamika maumivu sehemu za vidole vya
miguu yote, BAHATI BUKUKU (40) ambae ni mwimbaji wa nyimbo za injili na
mkazi wa Tabata – Dar es Salaam ambaye analalamika maumivu sehemu
mbalimbali za mwili wake.
Mwingine
ni FRANK CHRISTOPHER (20) mwimbaji pia wa nyimbo za injili mkazi wa
Tabata Dar es Salaam ambapo kapata michubuko usoni na mkono wa kulia.
Wote
wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa matibabu na hali zao
zinaendelea vizuri ambapo Kamanda Misime amesema walikuwa wanatokea Dar
es Salaam ambapo dereva alikuwa anelekea DRC – Kongo, BAHATI d/o BUKUKU
na FRANK s/o CHRISTOPHER walikuwa wanakwenda Kahama kwenye tamasha la
Injili.
Uchunguzi wa ajali hii unaendelea ikiwa ni pamoja na kutafuta gari lililowagonga.
No comments:
Post a Comment