02 June 2014

VIDEO MPYA YA DIAMOND IMEGHARIMU MILIONI 70 ZA KITANZANI

KICHUPA (video) kipya cha mwanamuziki wa Tanzania Diamond Platnumz, alichorekodia London, Uingereza, kimemgharimu zaidi ya Sh70 milioni kutayarisha licha ya audio ya wimbo huo kutengenezewa Nigeria miezi miwili iliyopita.
Mteule huyo wa tuzo za BET ambaye amemshirikisha mwanamuziki Iyanya kutoka Nigeria katika wimbo huo, amesema video hiyo imemgharimu fedha nyingi, ambazo ameamua kuwekeza katika muziki huku akiamini atavuna fedha nyingi kupitia muziki wake.
Diamond anasema anaumia sana pindi anapokuwa akifanya kazi zake kwani huchukua kiasi kikubwa cha fedha na kuwekeza katika muziki ili kukuza bongofleva na kuutangaza muziki wa Tanzania.
 Si kwamba ninafanya hivi kama Diamond, la hasha! Bali ninafanya kwa mapenzi ya Tanzania. Lazima nihakikishe naendelea kuipeperusha bendera ya nchi yangu ili hata wageni wanaonijua sasa waone dogo sikubahatisha
anasema Diamond.
Anasema alitumia Dola 25,000 pekee kumlipa prodyuza wa video hiyo, kwani alitakiwa amfuate London yalipo makazi yake.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname