
Nabii anayetikisa kwa maono ya vitu mbalimbali Hosea Chamungu 'Mzee wa maono' ameibuka na jambo zito baada ya kufunga kwa siku tatu mfululizo huku akifanya maombi nyikani......
Akiongea
na mwanahabari wetu mapema wiki hii, nabii Chamungu alisema
kuwa amekuwa na desturi ya kufunga siku tatu kila wiki ili
kupata maono ya mambo mbalimbali yanayojiri hapa duniani.....
Chamungu ambaye kabla ya unabii amewahi kuwa mwanachama wa
Freemasons amesema alichofunuliwa hivi majuzi ni kwamba bado
vifo vitaendelea kuwaandama wasanii mbalimbali na kabla ya
kumalizika kwa mwaka huu wa 2014 kuna msanii mkubwa wa mziki
wa Bongo Fleva atafia jukwaani.....
"Atafariki kwa ajili ya pesa na itakuwa jukwaani, yawezekana
akawa anagombea pesa au anatunzwa pesa jukwaani ndipo umauti
utakapomkuta," alisema Chamungu huku akisisitiza kuwa hayo ni maono na si hadithi.
Chamungu alifafanua kuwa vifo vinavyohusisha pesa hutokana na
shetani ambao ni jamii ya Lucifer na Illuminati ambapo pia
hujulikana kama Freemasons....
"Kifo chake kitavuta hisia za watu wengi wakiwemo wakawaida
na maarufu kama ilivyotokea kwa marehemu Kanumba lakini
hatazikwa na watu wengi kama alivyozikwa Kanumba," alisema
No comments:
Post a Comment