Video vixen Agnes Gerald a.k.a Agnes Masogange amefunguka kuhusu
matatizo aliyoyapata mwaka jana baada ya kukamatwa uwanja wa ndege wa
Or-Tambo, Afrika Kusini (July 5 2013) na mzigo uliosemekana kuwa ni dawa
za kulevya.
Agnes ni miongoni mwa Watanzania waliokwenda Durban, Afrika Kusini kumsupport Diamond Platnumz katika Tuzo za MTV (MAMA) weekend iliyopita, na Bongo5 ambayo pia ilihudhuria Tuzo hizo ilipata nafasi ya kufanya nae Exclusive Interview.

“Ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kuingia jela sijawahi kuingia jela
tangu nizaliwe, nilivyoingia mle ndani nikawa naomba kila siku eh Mungu
wangu,” alisema Aggy.
Pamoja na mengine, Masogange ambaye kwa sasa amehamishia makazi yake jijini Johannesburg, aliweza kushare na sisi jinsi maisha yake ya jela yalivyokuwa baada ya kukamatwa na kuwekwa ndani huko Afrika Kusini. “Nilivyofika pale na watu walivyokuwa wanachukulia yani na mimi nilikuwa nahisi labda siwezi kutoka leo wala kesho, nilikuwa nahisi labda ntapigwa sentence ya miaka kumi miaka kumi na tano lakini Mungu ni mkubwa nimetoka.” Alisema.

No comments:
Post a Comment