14 June 2014

BREAKING NEWS: MJUMBE WA HALMASHAURI KUU TAIFA-NCCR MAGEUZI ATEREKEZWA NA CHAMA CHAKE BAADA YA KUPATA AJALI



TAARIFA KWA UMMA JUU YA KUTEREKEZWA NA CHAMA CHANGU.
Ndugu Watanzania na wale wote wanaojali UTU wa mtu, kwa kweli leo imenibidi niseme tu kutokana na hali yangu inavyozidi kuwa mbaya kutokana na chama changu NCCR-Mageuzi kunitelekeza baada ya kupata ajali nikiwa nasimamia uchaguzi wa mdogo wa marudio wa udiwani huku mimi nikiwa mwandamiz wa chama kitengo cha vijana wa NCCR-Mageuzi mwaka jana 2013 kabla sijawa Mjumbe wa Halmashauri kuu mwaka 2014..

Uchaguzi mdogo wa mwaka jana 2013 wa udiwani kata ya Nyampulukano wilayani Sengerema tulipata ajali jumamosi ya kuamkia uchaguzi tukiwa na viongozi wa jimbo la Sengerema mimi nikiwa mbele tukitoka kukagua vituo vya kupigia kura baada ya kuambiwa vimehamishwa na nikiwa ndio msimamizi mkuu wa uchaguzi huo.

Ajali hiyo ilisababisha nipate maumivu makali lakini viongozi wangu wakatibu gari tu na kuacha kutibu mwili wa binadamu. Swala hili hata siku ya uchaguzi mkuu wa chama januari mwaka huu2014 ndani ya ukumbi wa diamond Jubilee nililisema lakini mpaka leo sijasikilizwa wala kuhudumiwa na chama hata kufikiriwa nikiendelea kuteseka na huku familia yangu ikiumia hasa wanangu na mke wangu.

Ombi langu kwa Serikali na asasi za kirai naomba msaada wenu ili nikachunguze afya yangu kwani inazidi kuwa mbaya.

Nasikitika sana mfumo wa upinzani kama vijana tunaumia kazini lakini hatujaliwi unadidimiza imani ya Taifa kwa Vijana na kujenga kukosa imani na Upinzani.

Kipimo cha Mwanasiasa Bora ni kujali Utu.

Mwanasiasa asiyejali utu sio mwanasiasa ,sio mtu mwema bali ni adui wa wale anaowa-inspire,ni adui wa wale anaowaongoza,ni adui wa jamii na Taifa ambalo linajali misingi ya utu katika kujenga taifa lililostarabika linalojali haki

Tusisite kutangaza vitaya kutetea haki zetu dhidi ya wanasiasa wa aina hii na Mungu ambaye Wengi wanamsujudia atakua nasi.Najua wengi Mmeumizwa/Tumeumizwa.Naelewa Maumivu haya ambayo baadhi yetu tumepitia,tunaendelea kuyapitia na kitu bora zaidi -Tuyatarajie.

Maisha yetu halisi yawe mfano wa kile tunachopigania.Tuwe principled.Hii ni kwa wote bila kujali itikadi zetu.

Ndugu wanahabari naiomba Serikali inasidie kwani sina jinsi nami nimeshatelekezwa ninatembea nikiwa nimeshaumizwa bila matibabu sitahiki.


DEOGRATIUS KISANDU
MJUMBE WA HALMASHAURI KUU TAIFA-NCCR MAGEUZI.
0786 025 609
13/06/2014

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname