Mlipuko
kadhaa imetokea mjini Mombasa nchini Kenya, ambapo imedaiwa walipuaji
wamelipua sehemu tatu tofauti. Akizungumza kutoa taarifa za tukio hilo
Kamishna wa kaunti ya mombasa Nelson Marwa, amesema kuwa waliotekeleza
shambulizi hilo huenda wametoroka wakitumia piki piki.Aidha amesema kuwa
watu 3 wamefariki kutokana shambulizi hilo la guruneti, huku mlipuko
mwingine ukishuhudiwa katika eneo la Nyali Reef, lakini hakuna majeruhi.
Ikumbukwe
kuwa shambulizi hili linajiri siku chache tu baada ya mlipuko mwingine
kushuhudiwa jijini Nairobi katika kituo cha polisi cha Pangani ambapo
watu 4 wakiwemo maafisa 2 wa polisi walifariki.
Walijeruhiwa
25,kwa sasa waliojeruhiwa wanaendelea na matibabu ikiwa ni pamoja na
xray na ukaguzi mwengne.viongozi wa kaunti wa msa wamefika.
No comments:
Post a Comment