09 May 2014

RAY C AFUNGUKA KUHUSU KUNUSURIKA KIFO KWA GONJWA HATARI LA DENGUE..

Staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’.
MUNGU mkubwa! Staa wa muziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amesimulia jinsi alivyochungulia kifo baada ya kutikiswa na ugonjwa hatari na tishio ulioibuka hivi karibuni wa Homa ya DengueAkifunguka mbele ya gazeti hili juzi baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini Mwananyamala, Dar alikokuwa amelazwa, Ray C au Kiuno Bila Mfupa alisema kwamba kwenye maisha yake hajawahi kushikwa na ugonjwa wenye mateso makali, tena ya muda mfupi kama ilivyokuwa juzikati alipopata ugonjwa huo.

Alisema kwamba dakika chache tu baada ya kuamka kitandani alikuwa akijisikia kichwa kikiuma kama kinataka kuchomoka ambapo bila kuremba aliwasha gari lake na kukimbilia Hospitali ya Mwananyamala.Staa huyo wa Ngoma ya Na Wewe Milele alisema alipofika kwa kudra za muumba alilazwa tayari kwa kutundikwa dripu. Inaendelea >>>>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname