08 May 2014

PICHA::MSANII DR CHENI ALAZWA HOSPITALI HOI KWA UGONJWA WA DENGUE


Dr Cheni akiwa hospital Msanii wa filamu nchini, Dr Cheni amelezwa toka jana katika hospitali ya Buruhani jijini Dar es Salaam kutokana na ugonjwa wa Dengue.Akizungumza na mtandao wetu leo Dr Cheni amesema kuwa bado hali yake sio nzuri kutokana na kuishiwa damu na mwili kupoteza nguvu.
“Bado ni nipo hospitali ya Buruhani naumwa hili gonjwa jipya,sijui unaitwa Dengue,” amesema. “Bado hali yangu sio nzuri kabisa,yaani naumwa,napungukiwa damu,mwili unauma,kwahiyo yanai bado ninaumwa,hii homa ilinianzia wiki iliyopita sema nilikuwa bado hawajaigundua ila jana ndio wameingundua,” ameongeza.
Dr Cheni amesema kuwa anawaomba Watanzania wamuombee kwani bado hali yake sio mzuri.

Dr Cheni akipewa huduma na msanii mwenzake wa filamu

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname