Staa
wa hiphop kutoka Marekani Wiz Khalifa (26) Jumapili ya May 25 2014
amedakwa na polisi katika uwanja wa ndege huko Texas Marekani baada ya
kukutwa na kitu kinachodaiwa kuwa ni dawa za kulevya aina ya bangi
kwenye mizigo yake zipatazo 200.
Alikuwa
akisafiri kutoka El Paso kwenda Dallas wakati maafisa wa uwanja wa
ndege walipokuta mzigo huo ndani ya begi lake ambapo kwa mujibu wa
sheria aliwekwa kizuizini na baadae kufikishwa kituo cha polisi kabla ya
kuachiwa huru saa kadhaa baadae kwa mujibu wa TMZ.Pamoja na hayo, yeye mwenyewe Wiz hakuonyesha kujali ambapo baadae alitweet picha yake akiwa chini ya ulinzi na kuonyesha hiyo ishu haijamsumbua akili kabisa
Alipokua chini ya huo ulinzi kwa saa kadhaa Khalifa alitweet na kuonyesha picha zake akisisitiza pia kuachiwa huru.
Hiyo
ndege binafsi ya kusafiria kwenye picha ya kwanza hapo juu ndio
inaaminika aliitumia kusafiri muda mfupi baada ya kuachiwa huru na
kupiga picha akiwa pembeni yake kuthibitisha kwamba aliachiwa huru.
Alipoulizwa
na shabiki wake kama alipata mateso yoyote alipokua chini ya huo
ulinzi, Khalifa alijibu kwamba kila kitu kilikua poa, yani alikaa vizuri
tu bila matatizo.
Staa
huyu aliefanya mpaka bongo imfahamu kwa sana kupitia single yake ya
‘Black and Yellow’ hii ni mara yake nyingine kukamatwa na bangi ambapo
kisa kingine kilitokea November mwaka 2010
No comments:
Post a Comment