02 May 2014

MTOTO ATAKA KUMUUA BABA YAKE HUKO MWENGE JIJINI DAR

Baba mzazi wa Anord Michael aliyedaiwa kutishiwa maisha na kijana wake

Katika tukio la kushangaza, kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Anord Michael mkazi wa Mwenge jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki iliyopita alifanya vurugu kubwa nyumbani kwao, akidaiwa kutaka kumuua baba yake mzazi kwa sababu ambazo hazikueleweka sawasawa. 

Huku majirani na watu wengine wakishangazwa na kitendo hicho, Anord alimfungia ndani baba yake mzazi na kuanza kumshambulia kwa silaha mbalimbali kabla ya kuchukua panga kwa lengo la kutaka kummaliza kabisa.


Polisi wakimdhibiti kijana Anord Michael




 Mzee Michael, kuona kijana wake amepania kummaliza, alipiga mayowe ya kuomba msaada, kitu ambacho kilifanikiwa kwani mara moja wasamaria wema walijitokeza na kumuokoa kwa kumhifadhi katika chumba kingine ndani ya nyumba hiyo. Endelea hapa >>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname