Lanjui
aliyelazwa katika Wodi Namba Nne katika hospitali hiyo tangu Januari
Mosi, 1971, awali alilazwa katika Hospitali ya Sekou Toure, Mwanza
kuanzia mwaka 1969 mara baada ya kupata ajali.
SINGIDA. Usiombe
yakupate. Abdi Lanjui (75), ametimiza mwaka wa 45 akiwa wodini katika
Hospitali ya Mkoa wa Singida alikolazwa tangu mwaka 1971 baada ya kupata
ajali ya lori.
Lanjui
aliyekuwa dereva wa taasisi aliyoiita “Mamlaka ya Pamba,” alipata ajali
hiyo mkoani Mwanza baada ya lori alilokuwa akiendesha kuchomoka gurudumu
la mbele na kupinduka.
“Sababu
ya mimi kugeuza wodi kuwa makazi yangu ya kudumu ni ajali
iliyosababisha kupooza kuanzia kiunoni hadi kwenye nyayo. Kwa kuwa
sinyanyuki kitandani, nimepata vidonda kuanzia makalioni hadi miguuni.
Kwa sasa naishi maisha magumu mno,” alisema. Aomba msaada Kutokana
na hali hiyo, ameiomba Serikali na jamii kwa jumla kumsaidia chakula
kwa kuwa hana ndugu wa kumsaidia. Lanjui ambaye hawezi kunyanyuka
kitandani, alisema kwa miaka mingi uongozi wa hospitali ya mkoa ulikuwa
ukimhudumia kwa kumpa chakula lakini baadaye huduma hiyo ilisitishwa,
hivyo kumfanya awe ombaomba na maisha yake kuwa ya mlo mmoja kwa siku.
No comments:
Post a Comment