Watu
mbalimbali wenye magonjwa wakimiminika kwenye maji ya bwawa nchini
Nigeria na kuoga wakiwa na imani ya kuponywa magonjwa yao.
WANADAMU wanazidi
kuegemea kwenye imani utata! Hivi karibuni, watu mbalimbali wenye
magonjwa wamekuwa wakimiminika nchini Nigeria na kuoga maji ya bwawa
yanayodaiwa yanaponya magonjwa papo hapo.Watu hao wakiwemo wazee,
vijana waume kwa wake na wenye magonjwa mbalimbali wamekuwa wakizama
kwenye maji hayo kwa urefu wa futi tatu hadi nne, wengi wakiwa uchi au
nguo za ndani tu.
Wengine huchota maji hayo na kuosha sehemu yenye tatizo hasa wale wenye kushindwa kuona au wenye vidonda sugu kama vile kansa, Ukimwi nakadhalika.
Wengine huchota maji hayo na kuosha sehemu yenye tatizo hasa wale wenye kushindwa kuona au wenye vidonda sugu kama vile kansa, Ukimwi nakadhalika.
Bwawa
hilo limepewa jina la Orimiri lipo umbali wa kilomita 3 kutoka mji wa
Nachi, Enugu nchini humo na liligunduliwa na watu wa Kabila la Fulani.
Tangu kugunduliwa kwa bwawa hilo, zaidi ya watu 3000 wameshafika kuyaoga maji hayo kuanzia asubuhi hadi saa 12 jioni.Soma zaidi
No comments:
Post a Comment