Kamishna kova ambaye amezungumza na
wanahabari muda mfupi uliopita
Kati ya watuhumiwa 149 waliokamatwa mmoja
amegundulika kuwa ni kiongozi aitwaye ATHUMANI SAIDI miaka 20, Mkazi wa Kigogo
na amekiri anaongoza kundi la watu zaidi ya 15 ambao baadhi yao ni kati ya
waliokamatwa.
Imegundulika pia kwamba vijana hawa
wanatumia dawa za kulevya aina ya bangi na wengine hujichoma sindano na
kuwafanya iwe rahisi kujihusisha na matukio ya uhalifu. Vijana hao hupenda kushiriki katika ngoma
kama Mnanda, Mchiriku, Kigodoro, Kanga moja nk. ambazo kwa kawaida huchezwa
hadi usiku wa manane.
Wakitoka katika ngoma hizo hujikusanya
pamoja na kufanya matukio ya uporaji kwa mtu wanayekutana naye, kufanya
uvunjaji katika majumba na wakati mwingine wana mtindo wa kugema mafuta ya
diesel au petrol katika matanki ya malori yanayosafirisha mafuta.
Operesheni kali inafanyika katika
maficho ya wahalifu hao ikiwa ni pamoja na daraja la River side, Kigogo
darajani, Manzese, maeneo ya Tandale pamoja na maeneo mengine ya maficho mkoa
wa Kipolisi Temeke.
Tunawasiliana na Maafisa utamaduni wa Wilaya zote za Mkoa wa D’Salaam
kusimamisha utoaji wa vibali wa ngoma za usiku ambazo hazina tija. Pia Jeshi la Polisi linafuatilia na kuwavizia
vijana wanaopora watu wanaotoka katika
sherehe za usiku kama vile Harusi na wanaotoka katika mikesha ya Ibada na
sehemu zozote zenye mikusanyiko.
Aidha Jeshi la Polisi wanapambana na vijana wanaowavizia watu katika
vituo vya mabasi pindi wanapotoka alfajiri kwenda katika shughuli zao za kila
siku.
Zipo taarifa kwamba baadhi ya wazazi
wasio waaminifu wamewasafirisha watoto wao wahalifu katika makundi haya kwenda
mikoani ili kukwepa wasinaswe na msako huu mkali. Hata hivyo Jeshi la Polisi lina mtandao wa
kutosha kati yake na mikoa mingine na nchi jirani hivyo litawatafuta popote
walipo na kuwakamata.
Oparesheni hii ni endelevu na ya
kudumu hadi kero hii ya vibaka itakavyokwisha kabisa. Baadhi ya majina
waliokamatwa ni kama ifuatavyo:-
1.
DANIEL PETER @ MALUNDE, miaka 25, mkazi wa Yombo Kigunga
2.
MWISHEHE ADAM, miaka 35, mkazi wa Mtoni mashine ya maji
3.
MOHAMED SAID, miaka 32, mkazi wa Mtoni
4.
JAKAMA ALPHONCE, miaka 23, mkazi wa Mtoni Kilakala
5.
HAMADI MDUDU, miaka 25, mkazi wa Mbagala
6.
SALUM MUSA, miaka 25, mkazi wa Kiwalani
7.
ANTHONY DANIEL, miaka 20, mkazi wa Mashine ya maji
8.
FIDELIN ANTHONY, miaka 18, mkazi wa Kigogo
9.
HAMZA MAZUMA, miaka 19, mkazi wa Kigogo
10. MGANGA ABEID, miaka 20, mkazi wa
Kigogo
11. SAID ABEID, miaka 19, mkazi wa
Kigogo
12. SALUM NYENJE, miaka 36, mkazi wa
Chamazi
13. DOMINICK PETER miaka 22, Mkazi wa Kigogo
14. KULWA ABEID, miaka 20, mkazi wa
Mabibo
15. MUSA IBTRAHIM, Miaka 20, mkazi wa
Magomeni
16. HUSSEIN SHABAN, miaka 22, Mkazi wa
Magomeni
S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM
|
No comments:
Post a Comment