WATU
wasiozidi 50 wamenusurika kifo baada ya basi dogo kupinduka katika eneo
la Sinai nje kidogo ya mji wa Songea mkoani Ruvuma kutokana na uzembe
wa abiria .Ajali hiyo ilisababisha na mtu mmoja ambaye anadaiwa kuwa ni
askari wa jeshi la kujenga Taifa JKT Mlale Songea ambaye alikuwa ni
mmoja wa abiria kuamua kuendesha basi hilo baada ya dereva wa basi
kutelemka na kumsaidia dereva mwenzake ambaye basi lake lilikuwa
limeharibika.Dereva wa basi lililopata ajali Bernad Bernad maarufu kwa
jina la Kichefuchefu alisema yeye baada ya kutelemka kwenda kumsaidia
dereva mwenzake alishangaa kuona gari lake linarudi nyuma likiendesha na
mmoja wa abiria kisha kupinduka baada ya abiria huyo anayedaiwa kuwa
ni mwanajeshi kushindwa kulimudu kuendesha .Bernad alisema kuwa mabasi
madogo matatu yalikodiwa na familia za askari wa jeshi la kujenga Taifa
Mlale ili kufika mjini Songea na kwamba wakiwa katika eneo la Sinai
ndipo basi moja lilikuwa na hitilafu ndipo mabasi yote yalisimama ili
kwenda kumsaidia mwenzao ili waweze kuendelea na safari ya mjini Songea.
“
Baada ya kutelemka nilishangaa kuona gari yangu inarudi nyuma kwa kasi
kisha ikaanguka ikiwa na abiria ambao walipata majeraha na kukimbizwa
katika hospitali ya Peramiho,mtu aliyesababisha ajali anayedaiwa kuwa ni
askari wa JKT Mlale mara baada ya ajali amekimbia msituni tulijaribu
kumkimbiza tumeshindwa kumkamata’’,alisema Bernad.
Hata
hivyo mwandishi wakati anapita katika eneo la ajali hakuweza kukuta mtu
yeyote aliyekuwepo kwenye ajali hiyo zaidi ya dereva wa basi
hilo,utingo na wapita njia ambao walitoa lawama kwa askari huyo
aliyeamua kuendesha gari wakati yeye alikuwa ni abiria na kusababisha
ajali kwa uzembe.
Credit: Kwanzajamii.
No comments:
Post a Comment