Mjengo wa
staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ uliopo Mbezi
Temboni-Salanga jijini Dar es Salaam umeingia kwenye lawama kufuatia
madai kwamba, unatumika kwa kutapeli watu wanaotaka kununua nyumba
maeneo hayo.
Kwa mujibu
wa chanzo chetu ambacho kina makazi jirani na nyumba hiyo, baadhi ya
watu wanaojiita madalali wamekuwa wakiwapeleka wateja kwa siri kwenye
nyumba hiyo ambayo haijaisha na kusema inauzwa na Lulu mwenyewe.
MCHEZO ULIVYO
“Baadhi ya madalali feki wamekuwa
wakiwaleta wateja wanaotaka kununua nyumba maeneo haya. Wakifika
wanasema Lulu anaiuza, wakiwa wameshaiona wanatoa fedha za usumbufu au
za kuwapoza wasipeleke watej wengine na kutoa namba feki ya Lulu ili
mteja ampigie.
“Wapo wateja walishanifuata na kusema wanampigia Lulu hapatikani, lakini waliponionesha namba yenyewe si ya Lulu.
“Siku moja
mteja mmoja aliletwa na dalali kuiona nyumba, akaipenda, akampa dalali
shilingi 300,000 za kumfanya asipeleke wateja wengine, akampigia Lulu
hakupatikana. Alipokuja kwangu nikaiangalia namba hiyo ilisajiliwa kwa
jina la Mwanahamis nani sijui,” kilisema chanzo hicho.
MAPAPARAZI WAJIFANYA WATEJA, MADALALI WASHTUKA
Mwishoni mwa wiki iliyopita,
mapaparazi wetu walijifanya wateja wa kuinunua nyumba hiyo na kwenda
kukutana na watu wawili waliodaiwa kuwa ndiyo madalali, Kitwana na
Mambeze ‘Mchopa’.
Baada ya
mazungumzo, madalali hao walidai kuwa, funguo za kuingia ndani ya nyumba
hiyo anazo mama Lulu (Lucresia Karugila) na alisema angefika siku hiyo
saa kumi jioni na kuwataka mapaparazi kurudi muda huo.
Wakati
mapaparazi wetu wanaondoka, dalali mmoja alisema: “Nyie kama mmekuja
kututega mmeliwa wenyewe, hapa hakuna mtoto wa kijijini. Wanaokuja hapa
kutaka nyumba wanajulikana, nyie mmetumwa.”
LULU ALISHAFIKA, HAJUI KITU
Sosi mwingine alisema hivi karibuni
alimuona Lulu akifika eneo hilo kwa ajili ya kuangalia nyumba hiyo
ambayo imesimama ujenzi lakini hakuweka wazi kama alikuwa na nia ya
kuiuza!
“Mimi mara
ya mwisho nilimuona Lulu eneo hili na gari lake, naona alikuja kuangalia
nyumba inaendeleaje na usalama pia. Mambo ya kuwa anaiuza hata siyajui
ingawa kweli hata mimi nimekuwa nikiwaona watu wakija,” alisema sosi
huyo ambaye hakutaka jina lake lichorwe gazetini.
Juzi, gazeti hili lilimsaka Lulu kwa njia ya simu kwa ajili ya kumuuliza kuhusu suala hilo ambapo, awali aling’aka, akasema:
“Wewe ndiyo
unaniambia kusema ukweli, sijui chochote. Naomba mnipe habari kwa upana
ilivyo maana nyie waandishi mara nyingi mnakuaga wa kwanza kujua habari
kuliko mhusika.”
Amani: Wewe Lulu sema ukweli tu, kama unaiuza. Nilichokwambia ndicho.”
Lulu: Kweli mimi siiuzi nyumba yangu wala sina wazo. Huyo aliyewapa habari awape kwa undani ili nijue.”

No comments:
Post a Comment