19 March 2014

Wawili wapoteza maisha katika ajali ya gari

Ajali mbaya imetokea jana jumanne(18) mida ya saa 8:00 mchana maeneo ya Asa Norte,umbali wa km 1 kutoka mjini Jaru kuelekea Porto Velho nchini Brazil.Ajali hiyo ambayo ilihusisha gari aina ya Fiat Uno lililokuwa likielekea Jaru liligongana uso kwa uso na  Lori aina ya Mercedes na hivyo kusababisha ajali mbaya sana iliyopelekea baadhi ya watu kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya.Gari hilo dogo aina ya Fiat Uno ndilo lililo haribika vibaya na likiwa na watu 3 ,ambapo dereva wa gari hilo aliyejulikana kwa jina la John Bosco mwenye umri wa miaka 67 alikufa hapo hapo  na mwanamke  mwingine alipoteza miguu yake katika ajali hiyo huku watu wengine wawili wakijeruhiwa vibaya. Majeruhi walichukuliwa na kupelekwa katika hospitali ya manispaa ya Jaru kwaajili ya huduma ya kwanza na baadae waliamishiwa katika hospitali kuu mjini PortoKwa mujibu wa dereva wa lori, Donizete aliyekuwa akielekea Jaru kutoka Mjini akihojiwa na maafisa usalama barabarani alikili kuhusika na tukio hilo kutokana na mwendokasi wa gari lake ambao ulisababisha ajali hiyo kutokea.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname