Stori: Gladness Mallya na Hamida Hassan
OOOH!
Zikiwa zimepita siku chache tangu staa wa filamu Bongo, Wastara Juma
kunusurika kifo baada ya kudaiwa kunywa sumu na baadaye kupata ajali,
anadaiwa kusumbuliwa na roho wa kifo.
Kupitia ukurasa wake katika Mtandao wa Kijamii wa Instagram, Wastara
aliweka picha za wasanii mbalimbali huku akimwelezea kila mmoja alivyo
na mwishoni mwa maelezo hayo alimalizia kwa kusema kuwa ameamua kusema
kabla hajafa kwani kifo hakiko mbali.
00Baadhi ya mastaa aliowaelezea ni Tamrina Poshi ‘Amanda’, Denis Swea
‘Dino’, Jacob Steven ‘JB’, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, Halima Yahya
‘Davina’, Riyama Ally, Salma Jabu ‘Nisha’.
Wengine ni Cloud, Lamata, Bondi, Msafiri Kondo na wengineo ambapo
baada ya kumuelezea kila mmoja, chini alikuwa akiandika ujumbe huu:
“Sababu ya kufanya hivi, sisi ni binadamu na kifo hakiko mbali, naweza nikafa kabla sijasema lolote kwa watu wangu.”
WASTARA ANASEMAJE?
“Niliandika maneno hayo ili
wasanii wote waliowahi kunitendea wema wajue kwamba wao ni watu muhimu
sana katika maisha yangu, wapo wengi lakini sikuweza kuwashukuru wote
kwa sababu wakati naandika hivyo nilikuwa kwenye hali mbaya sana.
“Unajua siku moja nitakufa maana kifo kiko karibu sana hivyo
watakumbuka maneno yangu hayo niliyoandika ya kuwashukuru,” alisema
Wastara.
Baada ya kuwaelezea kwa kuwaandikia waraka huo, mashabiki mbalimbali
waliopo kwenye mtandao huo walionekana kusikitishwa na maneno hayo na
kujikuta wakimuuliza maswali yasiyokuwa na majibu kwa wakati huo huku
wengine wakidai kuwa Wastara anasumbuliwa na roho wa kifo
No comments:
Post a Comment