HUJAFA hujaumbika. Hicho ndicho unachoweza kusema ukimuona na baadaye kumsikiliza Disnia Rajabu,32, mkazi wa mtaa wa Geza Ulole mkoani Tanga ambaye anaumwa uvimbe wa mguu kwa muda wa miaka 10 sasa bila kupata nafuu.Disnia hakuzaliwa na tatizo hilo, bali alilipata ukubwani, tena akiwa tayari ameshaolewa, lakini katika hali ya masikitiko makubwa, anadai mumewe alimkimbia mara baada ya kugundua kuwa yupo katika majaribu makubwa kabisa katika maisha yake.Na kutokana na kukimbiwa na mumewe, mwanamke huyo sasa anaishi na wazazi wake, ambao nao wana uwezo mdogo kiuchumi, hivyo licha ya kutopata matibabu ya uhakika, pia maisha yake yeye na watoto wake watatu ni ya kubahatisha, kwani mara kadhaa hukosa kula.
“Ni bora nisingezaliwa kwa mateso niliyonayo, sina raha kabisa duniani kwani nina miaka kumi nipo kitandani, huwa nalia wanangu wanaponijia na kunililia kuwa wana njaa hawajui kuwa sina uwezo wa kuwatunza,” anasema mama huyo.INAENDELEA
No comments:
Post a Comment