05 February 2014

MSIKILIZE JOKATE AKIELEZA JINSI ALIVYO MALIZA BEEF NA WEMA..NA KUMSAPRISE TSH.LAKI 6 JUKWAANI ARUSHA

Jokate Mwegelo aka Kidoti ameelezea jinsi ilivyokuwa mwishoni mwa wiki iliyopita, baada ya kumsurprise Wema Sepetu kwenye show ya msanii wake, Mirror iliyofanyika jijini Arusha.
page
“It was a surprise,” Jokate ameiambia Bongo5. “Alinialika two weeks ago lakini sikuwa na uhakika kama ntaweza kwenda kutokana na ratiba zangu lakini later on nikasema ngoja nisimjibu, sikuongea naye tena kitu chochote. Kwahiyo nikaamua mimi na rafiki zangu kwenda Arusha, nikaamua tu
kumsuprise. Hakujua kama tupo wala sikusema popote kwamba naenda,”ameongeza Jokate.
cbf9c9f88cc911e38e2912d966ff09f8_8
Wema na Jokate wakiwa kwenye show ya Mirror jijini Arusha
“It was crazy,” amesema Jokate kuelezea ilivyokuwa baada ya yeye kupanda jukwaani. “It was nice though, kila mtu aliappreaciate, nadhani hicho ndio kitu kilichokuwa muhimu. I was also a bit nervous, sijawahi kufanya kitu kama kile na sikujua watu wataipokeaje but it was great. Kila mtu alifurahi, nadhani tumeipa pia heshima show yake.”
499b368c8cdc11e3b554122b944cbca2_8
Wema na Jokate wakicheza muziki pamoja
Jokate amesema yeye na Wema walikuwa wameshaziweka tofauti zao muda mrefu kuanzia kipindi kile kwenye msiba wa baba yake Wema, mwishoni mwa mwaka jana.
“Kwasababu ulikuwa msiba sikuweza kuweka public kwasababu msiba ni kitu sensitive sio vizuri kuchukua advantage kufanya vitu vingine ambavyo havieleweki. Naweza kusema ile ndio ilikuwa public appearance ya kwanza,” amesema Jokate.
8285c9ac8cce11e3931d0e6209f07faa_8
Jokate amesema hakuna tena tofauti kati yake na Wema na siku za usoni wanaweza kushirikiana katika mambo mengi ya kazi.
“I like it cause kuna wasichana wengi they look up to us. Tuangalie zaidi kushirikiana kuliko kuwa na vitu ambavyo havieleweki na havina mtazamo mzuri kwenye jamii. Na mimi hasa hicho ndio kilinisukuma kwamba do something kwenye event yake, kuonesha tu kwamba tunaweza kushirikiana na kufanya vitu positive kwenye jamii.”
Msikilize zaidi hapo chini. SOURCE BONGO5

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname