Muimbaji wa Lofa, Top C amesema tangu atangaze kutaka kujiondoa kwenye label ya Candy n Candy ya Kenya, ameanza kupokea vitisho kutoka kwa wasanii waliosalia wanaomchimba mkwara asikanyage tena nchi Kenya.
Top C alikuwa akiongea na mtangazaji wa kipindi cha Street Bamiza cha Nuru FM ya mjini Iringa, Nelly Calocy Msamila aka Nelly B.
“Kuna dogo mwingine wa pale pale anaitwa Imrani ambaye yeye yupo karibu sana na bosi ndo alikuwa akielezaeleza sijui ‘utaona usikanyage show za Kenya’ mimi nikamwambia ‘mimi nilikuja Kenya ndo nikapatana na hii kampuni,” amesema Top C.
Amesema kampuni hiyo inamtaka arudishe gharama ilizotumia kwake lakini anadai hakuna gharama kubwa iliyotumika kwaajili yake na kuongeza kuwa kwa sasa hana mpango tena wa kuwa chini ya usimamizi wa kampuni nyingine.
“Sasa hivi ntafanya kila kitu kimpango wangu, wanazingua hawa washkaji ila kuhusu mambo hayo ntakuwa macho sana sasa hivi. Yaani tunaingia sehemu tu unakuta mtu anakuchekea pale mnapoanza kuonana na tayari ukishaingia kunakuwa issue tena.”
Top C amesema kwenye kampuni hiyo anayepewa kipaumbele peke yake ni Baby Madaha ambaye ana uhusiano na boss wa kampuni hiyo.
Credits:Bongo5
No comments:
Post a Comment