15 February 2014

HUU SASA NI ZAIDI YA UNYAMA TUBADILIKENI, SOMA HAPA UJUE MKASA HUU KWA KINA

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida mkazi wa Kijiji cha Nyabibuye Kakongo katika Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, Susuluka (16) anadaiwa kujeruhiwa vibaya usoni na bosi wake, Imani Paulo (36) kwa kung’atwa ng’atwa usoni na kisha kunyofolewa macho, pua na meno kubaki nje, kama ambavyo anaonekana pichani.
Tukio hilo ambalo tunaweza kulifananisha na dunia kuelekea kufika mwisho, limegusa hisia za watu wengi hasa wakazi wa Kibondo, huku wengine wakitokwa na machozi kutokana na kuguswa na ukatili ambao amefanyiwa kijana huyo.Tunaweza kufikiria kuwa tukio hilo ni sinema, lakini Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Venance Mwamotto, ameliambia Majira kuwa tukio hilo limetokea miezi miwili iliyopita.
Akizungumza na Majira katika mahojiano maalumu, Mwamotto, alisema kuwa kabla ya kijana huyo kujeruhiwa na bosi wake, alimtuma dukani ili akamnunulie soda.Aliliambia Majirakuwa baada ya kufika nyumbani alimkuta bosi wake akiwa amemkaba koo mbwa na kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata mbwa huyo, alianza kuhema akitoa ulimi nje.
DC Mwamotto alisema kuwa mtuhumiwa huyo ghafla alianza kuung’ata ulimi wa mbwa na kisha kumeza vipande jambo lililosababisha mbwa huyo kupiga kelele kutokana na maumivu.Aliongeza kuwa aliendelea kula vipande vya ulimi huo wa mbwa hadi alipoumaliza.
“Unaweza kusema kuwa ni uongo, lakini ni tukio la kweli kabisa kwani mshtakiwa huyo aliendelea kula ulimi wote wa mbwa, huku kijana huyo akiendelea kumshangaa bosi wake kutokana na kitendo hicho kilichosababisha mbwa huyo kufa,”Wakati akiendelea kumshangaa bosi wake ghafla alimrukia na kumkamata kwa nguvu na kuanza kumng’ata kama mtu anayetafuna hindi la kuchoma.SOMA ZAIDI

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname