22 February 2014

DEREVA BODABODA ANYONGWA NA MAITI YAKE KUTUPWA KWENYE UWANJA WA SHULE

Marehemu Musa na mkewe enzi za uhai wake.
Dereva wa Bodaboda aliyejulikana kwa jina la Musa Wambari, 25, mkazi wa Kitunda, jijini Dar es Salaam amekutwa amenyongwa na maiti yake kutupwa katika Uwanja wa Shule ya Abdu Juma huko Kivule.
Tukio hilo la kuhuzunisha lilitokea Februari 9, mwaka huu saa 4 usiku baada ya marehemu kukodiwa na watu wawili.
Imedaiwa na madereva bodaboda waliokuwa wakiegesha pikipiki zao eneo la Matembele na marehemu kuwa, siku ya tukio wakiwa eneo lao la kazi alifika kijana anayedaiwa kujihusisha na uhalifu aitwaye Jose akiwa na mwenzake aliyevaa suti.
Mmoja wa madereva hao aliyeomba hifadhi ya jina lake aliongeza kuwa, Jose na rafiki yake walitaka kukodi pikipiki lakini kwa vile walikuwa wakimfahamu kwamba alikuwa muhalifu walikataa ndipo wakaondoka.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname