Muonekano wa basi la Penguin mara baada ya kupata ajali ya kugongana na land cruser.(habari/picha na Eddy Blog Team)
Muonekano wa basi hilo.
Abiria walionusurika kwenya basi hilo wakitazama basi hilo mara baada ya ajali licha ya mvua kunyesha lakini walibaki kuduwaa.
Zaidi ya abiria 20 waliokuwa wakisafiri na basi la Penguin lenye namba za usajili T 947 BVQ kutoka Njombe kuelekea wilayani Makete mkoani Njombe wamenusurika kifo baada ya basi hilo kugongana na toyota landcruser pick up yenye namba za usajili T 999 ARP
Ajali hiyo imetokea jana Februari 22 majira ya saa tisa alasiri katika kijiji cha Mang'oto wilayani hapo na kupelekea baadhi ya abiria hao kupata majeraha madogo madogo na wengine wakitoka salama
Kwa mujibu wa mwandishi wa eddy blog ambaye ni miongoni mwa walionusurika kwenye ajali hiyo amesema imetokea kwenye kona iliyokuwa katika eneo hilo na kushuhudia abiria hao wakitoka kwenye basi hilo wakiwa hawaaamini kilichotokea kufuatia wengi wao kulala kwenye basi huku safari ikiendelea kutokana na mvua iliyokuwa ikinyesha
Mmoja wa manusura wa ajali hiyo ambaye alikuwa akienda kumuuguza baba yake anayeendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Ikonda Consolatha ambaye pia hakupenda jina lake liandikwe mtandaoni amesema alikuwa amelela lakini ghalfa aliamka kutoka usingizini bada ya kusikia kishindo kikubwa huku akisikia abiria wenzake wakipiga kelele
Kwa mujibu wa maelezo ya abiria hao wamesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa magari yote mawili pamoja na mmoja wao kupita eneo ambalo si lake (kuibia barabara) na hivyo kutokana na hayo ilikuwa ni vigumu kukwepa ajali hiyo isitokee hata kama dereva aliishuhudia toka mbali
Dereva wa Toyota landcuser iliyokuwa imetoka kupeleka mafuta kwenye minara ya simu wilayani Makete ambaye amezungumza na mwandishi wetu eneo la tukio amesema yeye alikuwa mwendo wa kawaida na alikuwa akipita upande wake lakini alifatwa na basi hilo na kudai kuwa ukweli wa chanzo cha ajali hiyo utafahamika pale askari wa usalama barabarani watakapofika eneo la tukio na kufanya vipimo vyao
Abiria wengi walitawanyika eneo hilo kutokana na mvua iliyokuwa ikinyesha huku magari yanayotoka na kwenda Njombe na Makete yakishindwa kupita kutokana na ajali hiyo kuziba barabara
Hadi mwandishi wetu anaondoka eneo la tukio majira ya saa 10 jioni askari walikuwa hawajafika eneo la tukio, lakini alikutana na gari lao njiani eneo la tandala likielekea eneo la tukio
Habari za uhakika baada ya polisi kufika na kufanya vipimo vyao utaipata hapa hapa kesho Jumatatu
No comments:
Post a Comment