03 January 2014

Tumsilaumu Jackie Cliff, tumlaumu aliyemfundisha kuvua samaki, fahamu uhusiano kati ya urembo na biashara ya unga

Jackie Cliff… mrembo wa haja niliyeanza kumfahamu kwenye video ya She Got A Gwan ya Ngwair. Ni msichana aliyeenda hewani na Mungu kampelea haswaa. Ukikutana naye huwezi kumwangalia mara moja ukaridhika, lazima ugeukE kumwangalia tena.
Nilipata bahati ya kumhoji mwezi September mwaka jana kwenye fashion show ya Ally Rehmtullah iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam na katika maongezi yetu kuhusu Ngwair na kazi yake kama mrembo wa video nikagundua kuwa, Jackie ni msichana mpiganaji asiyejali kitu.
Jackie The Boss Lady, ni msichana anayejulikana kwa kuishi maisha ya kifahari yakiwemo kuendesha magari ya gharama ambayo wengi yaliwapa maswali mengi, ni wapi anapata fedha hizo? Ni kweli fani ya urembo inalipa hivyo? Sijasahau pia kuwa aliyekuwa mume wake, ni miongoni mwa madon wa Dar na ambaye alifungwa kwa miaka kadhaa kwa shutuma zile zile za sembe. 
Huenda fedha alizokuwa akizitumia na kuziumiza roho za watu wengi zilikuwa za mume wake ama tayari alikuwa ameshaanza kufanya biashara hiyo haramu na ya hatari kabisa duniani.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname