Shirika
la ndege la Emirates linasifika kuwa na ndege za gharama na kifahari
duniani ambapo wanasema mpaka mwaka 2018, wanataka kuwa wanamiliki ndege
za abiria zaidi ya 320.
Mpaka mwaka 2010, wanasema Emirates
walikua wanasafirisha abiria elfu mbili mia nne kwa wiki kutoka Dubai
International Airport kwenda kwenye majiji 105 ndani ya nchi 62 duniani
ambazo ziko ndani ya mabara sita.
Mpaka mwaka 2010 pia, Emirates walikua wameajiri Wafanyakazi elfu
kumi na mia saba wanaotoka kwenye nchi mia moja ishirini duniani na
kwenye kutimiza kwao miaka 25, walitangaza faida yao iliyofikia dola za
kimarekani milioni 964.
Unaambiwa Terminal 3 kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa Dubai
ambayo ilianza kutumika mwaka 2008 baada ya kujengwa maalum kwa ajili ya
kutumiwa na shirika hili la Emirates peke yake, iligharimu dola za
Kimarekani bilioni 4.5 ikiwa ni jengo lililotajwa mwaka 2010 kuwa kubwa
kwa kipimo cha upana likiwa na over 1,500,000 sq. m. (370 acres) of space.
Picha zinazofata hapa chini ndio zinaonyesha baa ambayo iko ndani ya Emirates Airline
No comments:
Post a Comment