13 January 2014

MUNGU HAMTUPI MJA WAKE, SOMA HAPA SIMULIZI HII YA KUSISIMUA


Hali ikazidi kuwa mbaya na kila mpango nilioupanga nikaona ukienda tofauti na matarajio yangu, kazini kukawa moto nyumbani nako baba mwenye nyumba kanipa mkataba mpya na kuwa sasa nitatakiwa kulipa kodi ya mwaka na sio miezi mitatu tena.

Pale kazini nilikuwa nafanya kama kibarua na nilitamani na ilikuwa katika mpango wangu kuwa ule mwisho wa mwaka nirudi kijijini kwa wazazi kuwasalimia na mchumba wangu alikuwa mjamzito.

Kwa wiki chache niliona mwili unapungua nakosa ujasiri na kuona kila kitu kikififia na ndoto ya mtoto wangu mtarajiwa kupata matunzo mema ikianza kutoweka pia.

Sikuwahi kuwa au kuona mwanamke jasiri kama mpenzi wangu, kwani pamoja na maisha magumu niliyokuwa nayo naye akiwa hana kazi na anaishi kwa wazazi wake bado alikuwa masaada mkubwa kwangu kwa kunipa ushauri wenye nguvu kuwa nitafanikiwa tu na wala nisikate tamaa na nizidi kumtegemea Mungu kwa kumshirikisha mipango yangu kwa njia ya maombi.

Mara nyingi nilipenda kumsindikiza mpenzi wangu kliniki na baada ya kupewa huduma alipenda kupata soda ya baridii na chipsi kuku, hivyo mara kwa mara nilihakikisha napitia bar moja maarufu kwa kuku choma wa kienyeji.

Wiki hii ilikuwa ni kliniki ya mwisho kwa mpenzi kabla ya kujifungua, nikaomba ruhusa ya kutokwenda kazini na kuamua kwenda kumsindikiza tena.....

Mfukoni sikuwa na kitu na kwa kuwa nilijua lazima chipsi kuku itahusika nikapitia kwa rafiki yangu na kumwomba aniazime elfu tano nami nikawa na elfu mbili nikaona chipsi kuku robo ingemtosha.

Baada ya kuhudumiwa pale kliniki nikaondoka naye na kwenda pale bar na kisha akaagiza chipsi na mimi nikaomba soda moja.

Maongezi yakawa yanaendelea ingawa mimi akili ilikuwa juu ya maandalizi ya mtoto na hali yangu ya kifedha.

Mpenzi akanishtua na kusema mbona umetupa kizibo wakati wenzako wanagombania kupata bahati ya gari, bajaji,bodaboda, fedha tasimu na soda za bure kutoka katika mchezo wa bahati na sibu unaochezeshwa na kampuni hiyo ya soda?

Nikamwambia mie siamini hayo, akakidaka kile kizibo na kukifungua....

Sikuamini macho yangu kuwa nimepata bahati ya gari na wote tukaduwaa kwa furaha ingawa bado sikuwa na imani yoyote ile.

Wiki chache baadae nikapokea gari langu na kuamua kuliuza na kupata kiasi kikubwa cha fedha ambacho kimenifanya niwe na biashara yangu, kiwanja na nimeanza kujenga na namshukuru "Mungu"

Pia nimepata bahati kubwa kwani mtoto kazaliwa salama na ninamtunza sasa na mwakani baada ya harusi nitaweza kupata muda mwingi wa kuitembelea familia yangu kule kijijini.

Namshukuru Mungu kwa muujiza huu kwani amejibu maombi yangu na pia mpenzi wangu kwa kunipa moyo wa ujasiri.

Na bila kumjali na kumsindikiza kliniki nafikiri nisingeweza kupata bahati hii

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname