19 January 2014

MTOTO WA MIEZI MINNE AIBWA KANISANI LEO HII WAKATI MAMA YAKE AKIENDA KUTOA SADAKA

Na Gideon Mwakanosya, Namtumbo
 
KATIKA hali isiyo ya kawaida kwenye kanisa katoriki prokia ya Namtumbo jimbo kuu songea  Anna Migamba (17) mkazi wa kijiji cha matili wilayani mbinga amedaiwa kuiba motto wa jinsia ya kiume mwenye umri wa miezi 4 wakati mama yake alipokwenda kutoa sadaka.
 
Habari zilizopatikana jana ambazo zimezibitishwa na paroko wa parokia Paulo Chiwangu zilieleza tukio hilo limetokea jana kwenye ibada ya kwanza wakati Selina Kamoye mkazi wa Eneo la Luwinga ambaye ni mama mzaziwa mototo aliyeibiwa alipokuwa anatoa sadaka.
 
Padri Chiwangu aliiambia NIPASHE kuwa wakati tukio hilo linatokea yeye alikuwa anaendela kutoa ibada ghafla waumini walianza kupiga kelele baada ya katekista Maria Fusi kutangaza kuwa kama kunamuumini alichukua mototo bila kujua amrudishie mzazi ili aondoke naye kwenda nyumbani.
 
Alisemakuwa pamoja na kuwa katekista alikuwa ametangaza kanisani juu ya kupotea kwa mototo waangalizi wa kanisa walifanya mawasiliano na polisi kama taarifa ya awali ambapo baadaye inadaiwa polisi walilazimika kufanya msako mkali kwakufunga barabra ya kuelekea tunduru na kuelekea songea jambo ambalo lilileta mafanikio kwani mtuhumiwa alikamatwa akiwa na motto kwenye basi akielekea songea mjini.
 
Naye Selina Kamoye alieleza kuwa jana majira ya saa 12 asubuhi aliondoka nyumbani kwake akiwa amembeba mototo wake James Trerifor mwenye umri wa miezi 4, kuelekea kusali kwenye kanisa Katoriki Parokia Namtumbo ambako ibada ikiwa inaendelea wakati wa kutoa sadaka alimwomba jirani yake aliyekuwa amekaanaye  ili aende akatoe sadaka.
 
Alifafanua kuwa huyo msichana ambaye alikuwa amfahamu alikubali kumchukua mototo na baadaye ilipofika zamu yake kutoa sadaka aliondoka na kwenda kwenye eneo la chombo ambacho kilicho andaliwa kwa ajili ya sadaka  kisha alitoa sadaka yake.
 
Alieleza zaidi kuwa baada ya kutoa sadaka alirudi kwenye eneo la kiti alichokuwa   amekuwa amekaa ghafla alipata mshituko baada yakuto kumkuta msichana aliyekuwa amemkabidhi mototo  ndimbo alipotoka nje ya kanisa na kwenda kumtafuta bila ya kuwa na mafanikio.
 
Hata hivyo afisa upelelez wa makosa ya jinai mkoani Ruvuma Revocatus Malimi alipoulizwa na NIPASHE kwa njia ya simu alizibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo alidai kuwa imetokea jana ndani ya kanisa katoriki parokia Namtumbo wakati ibada ya kwanza inaendelea.
 
Malimi alieleza kuwa baada ya polisi kupata taarifa ya tukio hilo iliwekwa mitego kwa kuweka viziwizi kwenye barabara ya Tunduru na kwenda Songea mjini ambayo iliweza kuletwa mafanikio ambapo Anna Migamba mkazi wa kijiji cha matili polisi walifanikiwa kumkamata akiwa ndani ya bus nje kidogo ya mji wa namtumbo akielekea songea mjini huku akiwa amebeba mototo siye wake na kwasasa hivi anaendelea kuhojiwa na polisi.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname