28 January 2014

MASKINI MCD WA TWANGA PEPETA AFARIKI DUNIA

28 Jan 2014: Mpiga Tumba mahiri katika muziki wa dansi hapa nchini, Soud Mohamed, ambaye pia alifahamika sana kwa jina la MCD, na aliyekuwa bendi ya African Stars a.k.a Twanga Pepeta na baadae akahamia bendi ya Mashujaa Band, amefariki Dunia usiku huu katika hospitali ya KCM mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro. Taarifa hizo zimethibitishwa rasmi na Msemaji wa Bendi ya Twanga Pepeta, Hassani Rehani.
Tutazidi kupeana taarifa za msiba huu kwa kadiri zitakavyokuwa zikitufikia.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname