31 January 2014

MAAJABU: SOKWE ATAKIWA KUTAMBULIKA KAMA BINADAMU KISHERIA, MAHAKAMA ISIPOKUBALI ITASHITAKIWA.


Kikundi kimoja cha kutetea haki za wanyama nchini Marekani kimeitaka mahakama mojamjini New York kumtambua sokwe kama binadamu kisheria.

Kikundi cha Mradi wa Haki Zisizo za Binadamu (Nonhuman Rights Project) kimetaka sokwe mtu alitwae Tommy kupewa hadhi ya “ubinadamu kisheria” na hivyo anastahili kupata “haki muhimu ya uhuru wa kimwili.”

Kikundi hicho kinapanga kufungua kesi ya aina hiyo wiki hii kwa kiniaba ya sokwe wengine watatu wa mjini New York.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Uingereza, BBC, kikundi hicho kinataka sokwe hao wanne kuachiwa huru kutoka kwenye kizuizi chao.

Kimesema sokwe hao wanapaswa kupelekwa mahali mwanachama na Bustani ya Umoja wa Sokwe Watu wa Amerika ya Kaskazini, kikundi hicho kimesema.

Kikundi hicho kilifungua kesi mahakamani Jumatatu kwa niaba ya sokwe Tommy na ushahidi wa wanasayansi umehusishwa katika kesi hiyo.

“Tunatoa hoja kwamba sokwe ni wanyama wanye utawala wao - yaani, wana uwezo wa kujitegemea kuamua, wenye ufahamu binafsi, na wenye uwezo wa kuchagua jinsi ya kuishi maisha yao,” mwasisi wa kundi hilo, Steven Wise, aliliambia shirika la habari la Marekani, Associated Press

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname