MUIGIZAJI wa kike aliyetamba katika Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu,
Cecilia Sospeter ‘Mamtei’ ametoa kali ya aina yake baada ya kusema
hawajui wasanii kutoka Bongo Movie, Wema Sepetu na Jacqueline Wolper.
“Wolper ndiyo nani na huyo Wema ndiyo nani? Wala siwajui kabisa na ndiyo kwanza nawasikia kutoka kwako. Bongo Movie imevamiwa kwa sasa na ndiyo maana wengi wanaoonekana ni wafanyabiashara na si waigizaji,” alisema Mamtei.
Cecilia Sospeter ‘Mamtei’.
Muigizaji huyo aliyejifungua mtoto wake wa pili wiki kadhaa
zilizopita, aliyasema hayo juzikati alipokuwa akihojiwa na paparazi wetu
nyumbani kwake Kinondoni, jijini Dar na alipogusiwa kuhusu uwezo wa
Wolper na Wema, alitiririka:
“Wolper ndiyo nani na huyo Wema ndiyo nani? Wala siwajui kabisa na ndiyo kwanza nawasikia kutoka kwako. Bongo Movie imevamiwa kwa sasa na ndiyo maana wengi wanaoonekana ni wafanyabiashara na si waigizaji,” alisema Mamtei.
No comments:
Post a Comment