Jacqueline Wolper amesema kuwa, ana imani kubwa na mpenzi wake wa sasa
aliyemtambulisha kwa jina la G Modo akiamini atampoza machungu
aliyoyapata kutoka kwa mpenzi wake wa zamani, Abdallah Mtoro ‘Dallas’
huku akiwatahadharisha mashosti zake kutoleta shobo (kuwa mbali naye).
Akipiga
stori na paparazi wetu hivi karibuni, Wolper alisema anafikia hatua ya
kusema hayo kwa kuwa muda mfupi aliokuwa naye amegundua ni mwanaume
anayejitambua na anayeheshimu mapenzi ila akawataka mashosti zake
kutomsogelea.
“Tangu
niwe na huyu kijana nimekuwa ni mwenye furaha kubwa, nasahau hata yale
machungu niliyopata kwa mpenzi wangu wa zamani. Lakini najua wapo
wanaomtolea macho, tusitafutane ubaya, kila mtu na maisha yake,” alisema
Wolper
No comments:
Post a Comment