22 January 2014

HII NDO JEURI YA PESA YA MWANAMUZIKI KOFFI OLOMIDE BAADA YA KUNUNUA GARI LA KIFAHARI LA BEI MBAYA

Ukiwataja wanamuziki matajiri basi Koffi ni mmoja wao, akiwa anamiliki 5 Star Hotel na akiwa na hisa kwenye kampuni kadhaa ndani ya Congo na nje ya Congo Koffi anaorodheshwa kuwa ni mmoja wa wanamuziki ambao wamefaidika vilivyo na muziki wao.

Majuzi Koffi aliingiza gari mpya Model ya 2012 aina ya Rolls Royce Phantom na kuitambiulisha kwa mashabiki.

Pichani Koffi Olomide akiwa mbele ya gari yake. Koffi ametangaza kung’atuka kwenye shughuli ya Muziki baada ya kutoa albamu yake mpya ambayo iko studio kwa sasa, Hii itakuwa ni Albamu ya 20 ya mwanamuziki huyu ambaye anamaliza akiwa na mafanikio na mpaka sasa albamu zake tatu zimeorodheshwa kwenye listi ya albamu 1000 ambazo unapaswa kusikiliza kabla ya kuondoka duniani (kufariki).

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname